Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Mlinzi wa kikosi cha kulinda amani Sudan Kusini kutoka China akiwa anashika doria mjini Juba.Picha
UNMISS(Picha ya Maktaba July 2018)

Idara ya zimamoto mjini Juba Sudan Kusini yaishukuru UNMISS kwa msaada wake wa magari

Mamlaka mjini Juba Sudan Kusini zimeushukuru Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS ambao umetoa msaada wa magari mawili makubwa ya huduma za uzimaji moto katika nchi hiyo ambayo miundombinu yake na huduma za kijamii vimeharibiwa na vita ya wenyewe kwa wenyewe iliyodumu kwa takribani miaka mitano.

Sauti
2'57"
Wakati wa mlipuko wa COVID-19 shirika la mpango wa chakula duniani WFP linagawa msaada wa kadi za fedha kwa familia 1,500 huko El Alto na La Paz, Bolivia
WFP/Morelia Eróstegui

Chakula ni dawa bora zaidi wakati wa mtafaruku:WFP

Mamilioni ya watu wako katika hatihati ya kutumbukia kwenye zahma ya njaa mwaka huu kwa sababu ya janga la corona au COVID-19 kwa mujibu wa shirika Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP, ambalo leo limetangaza mipango ya kuboresha kwa kiasi kikubwa operesheni zake za msaada wa chakula duniani ili kuwafikia mamilioni hayo ya watu.

Wahudumu wa afya katika kiliniki inayosaidiwa na UN karibu na kambi ya wakimbizi wa ndani ya Ceel Jaale katika eneo la Belet Weyne wakimuhudumia mama na bintiye mdogo.
UNSOM

Heko Somalia kwa upimaji wa COVID-19:UN 

Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia James Swan ameipongeza serikali ya Somalia kwa juhudi kubwa inazozifanya katika upimaji wa virusi vya corona au COVID-19 baada ya leo kuzuru maabara ya taifa ya afya ya umma (NPHRL) mjini Moghadishu.

Sauti
1'59"
Winnie Byanyima ambaye ni mkurugenzi mtendaji mpya wa UNAIDS akiwa kwenye moja ya mikutano ya kuwawezesha wanawake kiuchumi kwenye Umoja wa Mataifa.
UN Photo/Amanda Voisard

Huduma ya afya haipaswi kuwa biashara bali haki ya binadamu:Byanyima 

Mkurugenzi mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa linalopambana na ukimwi UNAIDS Winnie Byanyima amesema janga la corona au COVID-19 limeongeza adha kwa watu wanaoishi na VVU lakini pia kuyumbisha uchumi wa dunia na kuongeza pengo la usawa wa kijinsia, hivyo ameisihi dunia kuchukua hatua zinaozingatia haki za binadamu kama njia pekee ya kulidhibiti janga hilo.

Sauti
1'44"