UN yalaani mauaji katika jaribio la mapinduzi Ethiopia
Mauaji ya kamanda mkuu wa jeshi na gavana nchini Ethiopia katika kile serikali inachosema kuwa ni jaribio la kikanda la mapinduzi yamelaaniwa vikali na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Mauaji ya kamanda mkuu wa jeshi na gavana nchini Ethiopia katika kile serikali inachosema kuwa ni jaribio la kikanda la mapinduzi yamelaaniwa vikali na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema huu ni wakati wa mabadiliko , na kizazi chacke kimeanza kuelewa kwamba vijana wanaweza na wanapaswa kushika usukani .
Kamishina Mkuu wa Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa akizungumza katika mwisho wa ziara yake ya kwanza nchini Venezuela hii leo , ametoa wito kwa serikali ya nchi hiyo kuwaachilia watu wote wanaoshikiliwa kwa kuandamana kwa amani . Michelle Bachelet pia ametangaza kwamba timu kutoka ofisini kwake itasalia mjini Caracas mji mkuu wa nchi hiyo ili kufuatilia hali ya haki za binadamu
Watu wenye ulemavu wakumbukwe katika suala la utalii-Mbunge Tanzania. Mtu 1 kati ya 3 duniani hana fursa ya kupata maji safi ya kunywa na huduma za kujisafi- UNICEF/ WHO. Ili kukomesha ukatili wa ngono katika mizozo juhudi zaidi zahitajika:EU/UN. Matibabu ya kifafa bado ni shida kubwa kwa nchi za kipato cha chini- WHO. Nzige na Parara ndio chakula cha siku zijazo- Chef Ali
Takriban watu 3,340 wakiwemo wanawake, watoto na wanaume wamenufaika na mfuko wa Umoja wa Mataifa wa kusaidia manusura wa vitendo vya ukatili wa kingono vilivyofanywa na wafanyakazi wa umoja huo.
Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP limethibitisha hii leo kusitisha kwa kiwango kidogo mgao wa chakula kwenye maeneo yanayodhibitiwa na majeshi ya upinzani ya wahouthi nchini Yemen.
Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la chakula na kilimo FAO, limeanzisha kampeni ya kuchukua hatua madhubuti kuhakikisha kuna uendelevu katika uzalishaji na ulaji wa chakula.
Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS umekabidhi paneli 46 za kuzalisha nishati ya jua au sola na vifaa vyake kwa kituo cha redio cha Torit, 97.5 FM kinachoendeshwa na serikali ili kukipa uwezo na kuboresha operesheni za matangazo yake ambayo mara nyingi yanakatika kutokana na tatizo la umeme na mafuta ya jenereta.
Leo ni siku ya kimataifa ya Yoga ambayo inaadhimishwa na Umoja wa Mataifa kwa mwaka wa tano sasa. Mwaka huu 2019 maudhui ni “Yoga na hatua dhidi ya mabadilikoya tabianchi”
Mkutano wa 108 wa Baraza la shirika la kazi duniani, ILO ukikunja jamvi kwa kupitisha azimio la karne kufuatia shirika hilo kutimiza miaka 100, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amesema nyaraka hiyo ni fursa mpya ya kufungua mustakabali bora zaidi kwa wakazi wa dunia.