Mustakabali wa hali ya kazi uko katika maamuzi yetu ya sasa- Guy Ryder

10 Juni 2019

Mkutano mkuu wa mwaka wa shirika la kazi duniani ILO umeanza hii leo mjini Geneva Uswisi ukiwakutanisha wawakilishi wa serikali mbalimbali duniani, wafanyakazi na waajiri kutoka katika nchi 187 wanachama wa ILO.

Akihutubia katika ufunguzi wa mkutano huo wa 108 unaofanyika shirika hilo la kazi likiwa katika mwaka wa 100 tangu kuanzishwa, Mkurugenzi Mkuu wa ILO Guy Ryder amesema, “mstakabli wa kazi utakuwa matokeo ya maamuzi yetu, machaguo yetu, uwezo wetu wa kuyafuatilia, utashi wetu kushirikiana pamoja kufanya mstakabali wa kazi ambao tunautaka.”

Aidha bwana Ryder amewaeleza wajumbe wa mkutano kuwa wako hapo kwa sababu wana maono na ujasiri sawa na Albert Thomas ambaye alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa kwanza wa ILO na kwamba, “ni katika uwezo wetu kutengeneza masharti ya kazi bora kwa ajili ya wote, ambamo makampuni yatastawi, watu watafanikiwa na jamii zitaendelea. Hali ambayo inahakikishia kuendelea kwa maono ya miaka 100 ya waanzilishi wa ILO.”

“Mstakabali wa kazi, hautaamliwa kwa ajili yetu, siyo na roboti na siyo na akili bandia. Ukweli ni kuwa mstakabali wa kazi utakuwa matokeo ya maamuzi yetu.” Amesisitiza bwana Ryder.

Katika siku zinazofuata za mkutano huu, zaidi ya wakuu 40 wa serikali kutoka kote duniani watahutubia mkutano huo wa kimataifa wa 108 kuhusu kazi, ambao pia unafahamika pia kama bunge la la kazi la dunia.

 

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter