Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Mkuu mpya wa afisi ya UNAMID awasili Darfur

Mkuu mpya wa afisi ya pamoja ya Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa huko Darfur, UNAMIND, Profesa Ibrahim Gambari aliwasili mjini El Fasher, Darfur Jumatatu, na kukutana na maafisa wa makao makuu na kukagua gwaride la walinda amani katika jimbo hilo.

Mkutano wa Kimataifa juu ya Haiti unafanyika Montreal

Mawaziri wa mambo ya nchi za nje kutoka sehemu mbali mbali za dunia, akiwemo waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Hilary Clinton, wanakutana Montreal, Canada Jumatatu asubuhi, kwa mkutano wa kimataifa juu ya namna ya kusaidia kukarabati taifa la Haiti lililoharibiwa na tetemeko la ardhi.

UNCTAD: Uwekezaji wa Kigeni washuka sana mwaka 2009

Ripoti mpya ya Idara ya Biashara na maendeleo ya UM UNCTAD imegundua kwamba uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni FDI mwaka jana ulipungua katika kanda zote za dunia. Inaeleza kwamba mataifa yaliyoendelea yalishuhudia kuporomoka zaidi kwa uwekezaji mwaka 2008 na kuendelea kupunguka kwa mwaka 2009 kwa asili mia 41 zaidi.

Mswada una tishia kupunguza juhudi za kupambana na HIV Uganda

Mtaalamu maalumu wa UM kwa ajili ya masuala ya afya Anand Grover alionya Ijumaa kwamba mswada dhidi ya watu wa jinsia moja wanaopendana unaoanza kujadiliwa kwenye bunge la Uganda haukiuki tu haki msingi za binadamu za Uganda, bali utahujumu juhudi za kufikia lengo la kila mtu kupata huduma za kujikinga na HIV, matibabu na kusaidiwa.

KM asifu imani ya wanachi wa Haiti

Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-moon alisifu imani na ustahmilivu wa wananchi wa Haiti kufuatia tetemeko lililosababisha maafa makubwa wiki iliyopita, akisema ana amini kwamba, kwa msaada wa jumuia ya kimataifa wataweza kukabiliana na maafa hayo.