Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Hapa na Pale

KM Ban Ki-moon ametangaza taarifa yenye kulaumu vikali shambulio la bomu liliofanyika katika mji wa Lahore, Pakistan, ambapo watu 30 ziada waliripotiwa kuuawa na 250 wengine walijeruhiwa. Alisema hakuna kitendo chochote kinachohalalisha kosa hili la vurugu inayochochewa na ugaidi. KM aliwatumia mkono wa taazia aila za waathirika wa tukio hilo, na kuwaombea majeruhi wapone haraka, na kukukumbusha ushikamano uliopo baina yake na Serikali, pamoja na umma wa Pakistan, kwenye zile juhudi za kuwafikisha waliondeleza makosa haya mahakamani kukabili haki.

Utabiri wa DESA juu ya hali ya uchumi duniani kwa 2009

Idara ya UM juu ya Masuala ya Kiuchumi na Jamii (DESA) asubuhi iliwasilisha rasmi, ripoti ya katikati ya mwaka, yenye mada isemayo “Hali ya Uchumi Duniani na Matumaini kwa 2009”. Ripoti ilibashiria uchumi wa ulimwengu kwa mwaka huu utateremka kwa asilimia 2.6, baada ya huduma za kiuchumi kupanuka kwa asilimia 2.1 katika 2008, na baada ya kupanuka, vile vile, kwa karibu asilimia 4 kila mwaka katika kipindi cha baina ya 2004 na 2007.

ICRC inasema vita, maafa ya kimaumbile na bei ya juu ya chakula yaendelea kudhuru umma masikini duniani

Ripoti ya 2008 Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu (ICRC) iliowakilishwa mjini Geneva wiki hii na mkuu wa taasisi hiyo, Jakob Kellenberger, ilibainisha kwamba mamilioni ya watu walioathirika na hali ya mapigano duniani, waliendelea kumedhurika zaidi kimaisha kwa sababu ya mchanganyiko wa athari za vita, maafa ya kimaumbile na kupanda kwa bei za chakula kwenye soko la kimataifa.

Hapa na pale

Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) pamoja na Taasisi ya Mfuko wa Kimataifa kwa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) yamehadharisha ya kuwa mtindo wa wageni kumiliki ardhi za kizalendo - hususan katika bara la Afrika - ni tatizo linaloashiria wazalendo maskini huenda wakafukuzwa kutoka maeneo haya au kunyimwa uwezo wa kumiliki mali hiyo kuendesha maisha. Mashirika ya FAO na IFAD yameyahimiza Mataifa Wanachama kuhakikisha sheria za kumiliki ardhi kwa jamii zinazoishi kwenye vijiji zinahishimiwa, na kuwahusisha wenyeji hawa kwenye makubaliano yote yanayohusu biasahara ya kuwauzia wageni ardhi katika siku za baadaye .