Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Hapa na pale

KM Ban Ki-moon na Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu wameripotiwa kuchukuziwa na hotuba ya Raisi wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran, Mahmoud Ahmadinejad aliowasilisha Ijumatatu kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Mapitio ya Mwito wa Durban na Mpango wa Utendaji wa Kupiga Vita Ubaguzi wa Rangi Duniani uliofanyika Geneva, Uswiss.

Mkutano Dhidi ya Ubaguzi waanza rasmi Geneva

Mkutano wa UM juu ya Mapitio ya Mwito wa Durban dhidi ya Ubaguzi wa Rangi Duniani umeanza rasmi hii leo mjini Geneva. Kwenye risala ya ufunguzi, KM Ban Ki-moon alieleza masikitiko juu ya uamuzi wa baadhi ya nchi wanachama, wa kutohudhuria kikao hiki, licha ya kuwa ushahidi uliopo umethibitisha dhahiri kwamba ubaguzi wa rangi ni tatizo ambalo linaendelea kuselelea, na kujizatiti katika maeneo kadha wa kadha ya ulimwengu.

IFAD inasisitiza ruzuku kwa wakulima masikini ndio ufunguo wa kuuvua ulimwengu na mzoroto wa uchumi

Kanayo Nwanzeon, Raisi wa Shirika la UM juu ya Mfuko wa Kimataifa kwa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) ameyasihi mataifa yenye maendeleo ya viwanda kuharakisha misaada yao maridhawa kwa wakulima wadogo wadogo, hasa wale waliopo katika nchi masikini, ruzuku ambayo anaamini ikitekelezwa kidharura itasaidia sana kwenye zile juhudi za kuuvua ulimwengu na mzoroto wa uchumi uliotanda kimataifa sasa hivi.

Hapa na Pale

Navi Pillay, Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu amepongeza maafikiano yaliokamilishwa, kwa mafanikio, na Kamati ya Matayarisho ya Mkutano wa Mapitio Kuhusu Mwito wa Durban dhidi ya Ubaguzi wa Rangi.

JKK, Rwanda na UNHCR wajumuika kusailia taratibu za kurudisha makwao wahamiaji

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeripoti, kwa kupitia msemaji wake mjini Geneva, kuwa na matumaini ya kutia moyo, kufuatia uamuzi uliochukuliwa wiki hii na serikali za Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (JKK) na Rwanda, wa kukubali kuwasaidia raia waliohamia nchi mbili hiz kurudi makwao, kufuatia misiba kadha wa kadha iliolivamia eneo la Maziwa Makuu katika siku za nyuma.

Umma wa nchi masikini utafadhiliwa msaada wa tiba rahisi ya malaria

Kutoka mji wa Oslo, Norway kumeanzishwa rasmi, leo Ijumaa, ushirikiano mpya wa kimataifa wa kuwasaidia mamilioni ya watu wanaogua maradhi ya malaria duniani, hasa wale wanaoishi katika nchi za Asia na mataifa ya Afrika kusini ya Sahara. Mradi huu utawapatia umma huo uwezo wa kumudu dawa za tiba ya malaria, dawa ambazo hunusuru maisha ya mgonjwa, hususan wale watoto wa umri mdogo.

KM ametangaza sera mpya juu ya uhusiano wa kimataifa

Kwenye hotuba aliyoiwakilisha mbele ya wajumbe waliohudhuria warsha maalumu, leo asubuhi, katika Chuo Kikuu cha Princeton, kilichopo Jimbo la New Jersey, Marekani KM Ban Ki-moon alibainisha mtazamo wa sera mpya ya kimataifa juu ya uhusiano wa pande nyingi, miongoni mwa nchi wanachama.

Mashambulio dhidi ya viongozi wa Usomali yalaaniwa na UM

Ahmedou Ould-Abdallah, Mjumbe Maalumu wa KM kwa Usomali, amelaani vikali mashambulio ya karibuni yaliofanyika Mogadishu yaliowalenga wabunge, hujumu ambazo alisema zilikusudiwa hasa kuzorotisha juhudi za Serikali mpya ya Usomali za kupitisha Bungeni kanuni za Sharia, pamoja na kukwamisha zile jitihadi za kurudisha utulivu na amani ya eneo.