Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Wajumbe wa kimataifa wakutana Roma kuandaa miradi ya kudhibiti bora maji duniani

Wajumbe wa kimataifa kutoka nchi 60 ziada wanakutana mjini Roma, Utaliana kwenye Makao Makuu ya Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) kuanzia leo tarehe 21 mpaka 23 Januari (2009) ambapo wataendelea kujadiliana mpango wa utendaji, unaohitajika kudhibiti bora matumizi ya maji ulimwenguni, kufuatia athari mbaya za mazingira zinazochochewa na mabadiliko ya hali ya hewa duniani.

Vikosi vya Rwanda vyaruhusiwa na serikali ya JKK kuwasaka waasi wa FDLR

Shirika la Ulinzi Amani la UM katika JKK (MONUC) limetangaza rasmi kwamba wanajeshi karibu 2,000 wa Rwanda Ijumanne waliruhusiwa kuingia katika JKK, kwa kupitia eneo la mashariki, kuwasaka waasi wa Rwanda, wa kundi la FDLR, wenye asili ya kiHutu ambao inaripotiwa ndio miongoni mwa makundi yenye kupalilia hali ya wasiwasi kieneo kwa muda wa zaidi ya miaka kumi.

Hapa na Pale

Ijumanne KM ameripotiwa kutuma risala maalumu ya pongezi kwa kutawazwa kwa Barack Obama kuwa Raisi wa 44 wa Marekani. Risala hiyo ilisema KM ana “matarajio makubwa” kuhusu Uraisi wa Barack Obama kwenye zile juhudi za kutafuta suluhu ya mizozo kadha wa kadha ya ulimwengu iliokabili jumuiya ya mataifa: kama wasiwasi wa kiuchumi; athari za mabadiliko ya hali ya hewa; masuala magumu yanayohusu usalama na amani, ikijumlisha ukomeshaji wa uenezaji wa silaha za kinyuklia na upunguzaji wa silaha; pamoja na mchanganyiko wa matatizo yanayohusu mifumko ya bei za chakula na nishati na vile vile kupwelewa kwa huduma za maendeleo. KM alisema Raisi Obama ameahidi serikali yake ipo tayari kukabiliana na masuala haya bila shaka yoyote!~

Hapa na Pale

Mjumbe Maalumu wa KM kwa Eneo la MAziwa Makuu, Olusegun Obasanjo, Ijumanne alikutana na Raisi Joseph Kabila mjini Kinshasa katika JKK. Raisi Kabila alimweleza Mjumbe wa KM juu ya operesheni zinazoendelezwa shirika, sasa hivi, ndani ya nchi na majeshi ya JKK na Rwanda, dhidi ya kundi la waasi la FDLR. Operesheni hii zinatarajiwa kuendelea kwa wiki kadhaa zijazo. Vile vile mazungumzo ya kisiasa ya kudumisha suluhu ya amani kwenye Eneo la Maziwa Makuu, hususan katika sehemu ya mashariki katika JKK, bado yanaendelea chini ya usimamizi shirika wa Mjumbe Maalumu wa KM, Obasanjo na Raisi Mstaafu wa Tanzania Bejamin Mkapa. ~