Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari Mpya

Picha ya pamoja ya kikundi cha Washirika wa Maendeleo ya Kilimo na Lishe, wakulima, sekta binafsi, na watafiti na Taasisi za kitaaluma mjini Morogoro Tanzania.
UN News

FAO na wadau wawakutanisha wadau wa kilimo na chakula Tanzania

Nchini Tanzania, kwa ufadhili wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) na wadau wake kama Kitovu cha Kuratibu Mifumo ya Chakula cha Umoja wa Mataifa, Kikundi cha Washirika wa Maendeleo ya Kilimo na Lishe, wakulima, sekta binafsi, na watafiti na Taasisi za kitaaluma wamekutana mjini Morogoro ili kupitia na kuboresha vipaumbele na ramani ya mifumo ya chakula iliyoanzishwa mwaka 2021.

Chumba cha Mahakama ya Kimataifa ya Haki ICJ, huko The Hague katika kesi ya Afrika Kusini dhidi ya sraeli.
© ICJ/Wendy van Bree

Gaza : ICJ imeitaka Israel kukomesha mashambulizi dhidi ya Rafah mara moja

Mahakama ya kimataifa ya haki ICJ leo imetoa maamuzi ya kesi ya Afrika Kusini dhidi ya Israel iliyowasilishwa Mei 10 ikiitaka ICJ kuiamuru Israel isitishe mara moja oparesheni zake zote za kijeshi na kuwezesha upatikanaji wa misaada ya kibinadamu. Na tarehe 16 na 17 Mei,kuhusu utekelezaji wa Mkataba wa Kuzuia na Kuadhibu Uhalifu wa Mauaji ya Kimbari katika Ukanda wa Gaza.

Audio Duration
1'54"
UNICEF na wadau wake wasaidia kaya zilizoathirika na mafuriko zinapokea kwa kwa kuwapa msaada wa fedha taslim kupitia M-pesa na vocha za kielektroniki ili kuweza kujikimu na kimaisha.
UNICEF

Msaada wa fedha toka UNICEF unatusitiri baada ya mafuriko: Waathirika Garisa Kenya

Kenya inashuhudia kiwango kikubwa cha mvua zaidi ya kile cha kawaida ambacho kimesababisha mafuriko makubwa, maporomoko ya udongo na maelfu ya watu kutawanywa hivi karibuni. Miongoni mwa maeneo yaliyoathirika zaidi ni Kaunti ya Garisa , ambako hivi sasa asante kwa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na wadau wake kama shirika la Norway kwa ajili ya ushirikiano wa maendeleo NORAD, Mamlaka ya Kitaifa ya kudhibiti Ukame Kenya NDMA, na serikali ya Kaunti ya Garasa  kwani kaya zilizoathirika na mafuriko zinapokea msaada wa fedha taslim kupitia M-pesa na vocha za kielektroniki ili kujikimu kimaisha.

Sauti
3'11"