ILO yanusuru wanawake na mfumo wa utumwa nchini Niger
Nchini Niger mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kazi duniani la kujengea uwezo jamii zinazotumikishwa umeweza kunusuru maisha ya jamii hizo ambazo awali zilionekana hazina thamani kwenye jamii, lakini sasa sio tu zina uwezo wa kiuchumi bali pia zinatambua haki zao na kujua kusoma na kufanya mahesabu.