Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari Mpya

Bi. Salma Mukansanga, Mchechemuzi wa UNICEF kwa kipindi cha miezi 12 ili kusaidia utekelezaji wa Mkakati wa Uchechemuzi chini ya UNICEF Rwanda.
©UNICEF/Steve Nzaramba

Salima Mukansanga - Kama mimi nimefika Kombe la Dunia, hakuna ambako huwezi kufika

Michuano ya fainali za Kombe la Dunia kwa mchezo wa soka kwa wanaume inaendelea nchini Qatar huko Mashariki ya Kati. Mmoja wa watu wanaong’ara katika michuano hii ni Mchechemuzi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF Rwanda, Salima Mukansanga, ambaye ameweka historia ya kuwa mwanamke wa kwanza mweusi kuwa mwamuzi au refarii katika Kombe la Dunia. Aliingiaje katika tasnia hii ya mpira wa miguu? UNICEF Rwanda ilizungumza naye kabla hajasafiri kwenda Qatar na hapa Anold Kayanda anaeleza kwa lugha ya Kiswahili kilichozungumzwa. 

Sauti
2'39"
Virusi vya ndui ya nyani vinaweza kusambazwa kupitia malengelenge
© Harun Tulunay

Monkeypox au Ndui ya Nyani yabadilishwa jina sasa kutambulika MPOX

Baada ya mfululizo wa mashauriano na wataalamu wa kimataifa, hatimaye shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO litaanza kutumia jina MPOX badala ya Monkeypox au homa ya Ndui ya Nyani kufuatia mapendekezo ya kubadilishwa kwa jina hilo kwa maelezo ya kwamba lilikuwa linasababisha mambo kadhaa ikiwemo unyanyapaa. 

Sauti
2'24"
Wanawake katika kambi ya Dadaab nchini Kenya
UN Women

Wanawake Dadaab Kenya wajumuika kukabili misimamo mikali

Nchini Kenya shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake, UN Women kwa ushirikiano na wadau wanajengea uwezo wajenzi wa amani mashinani hata kwenye maeneo yenye changamoto kama vile kambi ya wakimbizi ya Daadab kwenye kaunti ya Garissa nchini humo kwa lengo la kuepusha vijana kutumbukizwa kwenye vikundi vyenye msimamo mkali.

Sauti
2'15"
Mwanamke akishiriki katika maandamano ya kupinga ukatili wa kijinsia huko Quito, Ecuador.
© UN Women/Johis Alarcón

Wanawake na wasichana ndio walio hatarini zaidi kuuawa majumbani: UN Women/UNODC

Ripoti ya utafiti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake UN Women na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya madawa na uhalifu UNODC inaonyesha kuwa wanawake na wasichana ndio walio katika hatari kubwa ya kuuawa majumbani, ikionyesha kuwa kwa wastani zaidi ya wanawake au wasichana watano waliuawa kila saa na wenzi wao au jamaa wa familia kwa mwaka 2021. 

Sauti
3'33"
Kikundi cha ushirika cha wanawake cha kuchakata dagaa nchini Senegal
UN Women/BrunoDemeocq

Uvuvi unasaidia mtu 1 kati ya 10 duniani , hebu tuboreshe maisha ya wavuvi:FAO

Ikiwa leo ni siku ya uvuvi duniani imeelezwa kuwa sekta ya uvuvi ni muhimu sana katika kuhakikisha uhakika wa kupata chakula na inasaidia mtu 1 kati ya 10 duniani kote. Kwa kutambua mchango wake wito umetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO kuboresha maisha ya mamilioni ya wanawake kwa wanaume wanaofanyakazi katika sekta hii kwa kuhakikisha haki zao za binadamu zinatimizwa.

Sauti
2'58"