Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari Mpya

Wanafunzi wakiwa darasani wilaya ya Kasese nchini Uganda.
© UNICEF/Maria Wamala

Msichana Manuela Christine kinara wa kuhamasisha wasichana kubaki katika shule Uganda  

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na wadau wake kwa kushirikiana na serikali ya Uganda, wanafanya juhudi kurekebisha athari ambazo zimeachwa na mlipuko wa ugonjwa wa Covid-19 hasa katika elimu ya watoto wasichana. Mmoja wa wadau katika mapambano hayo ni msichana Manuela Christine mwenye umri wa miaka 19 ambaye ni miongoni mwa wasichana wachache tu katika Wilaya ya Adjumani nchini humo ambao wanaendelea na elimu kwani takwimu za UNICEF na serikali ya Uganda zinaonesha takribani wasichana 32,000 walipata ujauzito kila mwezi katika miaka miwili ya kufungwa kwa shule.

Sauti
2'5"
Ahmad Hassan Yarow mwenye umri wa miaka 70 katika kambi ya wakimbizi wa ndani Luuq nchini Somalia
UN Photo/Fardosa Hussein

Katika umri wangu wa miaka 70 sijashuhudia ukame wa kiwango hiki- Mwananchi Somalia

Akiwa amesimama mbele ya kibanda chake kwenye makazi ya wakimbizi ya Kulmiye wilayani Luuq nchini Somalia, Ahmad Hassan Yarrow anatazama kile kilichosalia katika mto Juba, ambao ulikuwa ndio tegemeo la uhai wa  eneo lao. Mto umekauka. “Katika umri wangu wa miaka 70 sijawahi kushuhudia ukame kama huu, katika vipindi vyote vya ukame vilivyopita,” anasema Bwana Yarrow katika makala iliyochapishwa kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa usaidizi nchini Somalia, UNSOM.

Sauti
3'4"
Wanawake wakikimbia na watoto wakiingia Romani katika mpaka wa Siret.
© UNICEF/Alex Nicodim

Baadhi ya wakimbizi wa Ukraine wahamishiwa Romania kupunguza mzigo kwa Moldova

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, mamia ya wakimbizi kutoka Ukraine waliokimbilia Moldova, hasa wazee, familia zenye watoto wadogo na wanawake, wanapewa kipaumbele katika uhamisho wa kwenda nchi ya tatu, Romania kutoka Moldova kwa kuwa Moldova nchi iliyoko kwenye mpaka wa kusini mwa Ukraine ina rasilimali chache za kukabiliana na maelfu ya wakimbizi ambao wamevuka mpaka katika wiki za hivi karibuni.

Sauti
1'57"
Mwanaume akipima VVU kwenye kituo kimoja cha afya huko Odienné, nchini Côte d’Ivoire.
© UNICEF/Frank Dejongh

Sindano mpya ya Cabotegravir kusaidia kukinga wengi dhidi ya  VVU:UNITAID 

Shirika la Umoja wa Mataifa la kufanikisha upatikanaji wa dawa za tiba kwa gharama nafuu, UNITAID limetangaza utekelezaji wa mchakato mkubwa wa uvumbuzi wa hivi karibuni katika kuzuia virusi vya ukimwi ,VVU ambao ni sindano mpya  ambayo inachukua wiki nane kabla ya muathirika kupewa dozi nyingine badala ya tembe anazopaswa kumeza kila siku.

Sauti
2'25"