Walimu nchini Honduras huwa hatarini wanapoenda kufundisha shuleni
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema walimu nchini Honduras wanaathiriwa kwa kiasi kikubwa na ghasia za magenge ya wahalifu na sasa walimu wanatambuliwa kuwa moja ya makundi yenye uwezekano mkubwa wa kulazimika kuyakimbia makazi yao.