Mwaka 2022 tuazimie kujikwamua kutoka majaribuni- Guterres
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametuma salamu za mwaka mpya wa 2022 akitaka dunia iazimie kwa pamoja mwaka huu mpya uwe wa kuondokana na majaribu yanayotarajia kuikumba.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametuma salamu za mwaka mpya wa 2022 akitaka dunia iazimie kwa pamoja mwaka huu mpya uwe wa kuondokana na majaribu yanayotarajia kuikumba.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limekuwa na mjadala wa wazi kuhusu wanawake, amani na usalama ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema wakati umefika kwa baraza hilo kuonesha kwa vitendo uungaji wake mkono wa harakati za wanawake katika ujenzi na uendelezaji wa amani badala ya kusalia maneno matupu. Flora Nducha na maelezo zaidi.
Leo ni siku ya pamba duniani ikiwa ni maadhimisho ya kwanza kabisa ya siku hiyo kuenzi zao ambalo kitabaa chake kinatengeneza mavazi ya kila siku yaliyosheheni kwenye mkabati mengi ya nguo na ni kitambaa kizuri, rahisi kuvaa, kukitunza na kinadumu kwa muda mrefu. Lakini kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa thamani ya pamba ni zaidi ya kitambaa kama inavyofafanua taarifa ya Flora Nducha
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amehutubia mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hii leo kwenye makao makuu ya umoja huo jijini New York, Marekani ikiwa ni mara ya kwanza tangu ashike wadhifa huo mwezi Machi mwaka huu, huku akimulika masuala mbalimbali kuanzia uchumi, siasa, tabianchi, COVID-19 na usawa wa jinsia.
Mwanamke Mtanzania angara kituo cha safari za anga cha Marekani NASA tawi la Goddard mjini Maryland lililojikita na ufuatiliaji wa safari za satellite. Dkt. Alinda Mashiku ambaye amekuwa NASA kwa miaka minane sasa anasema ilimchukua miaka 12 hadi kuajiriwa NASA kama mhandisi na sasa pia ni meneja wa kitengo cha kuhakikisha satellite zonazokwenda angani hazigongani. Je anahisi vipi kuwa miongoni mwa wanawake wachache wahandisi NASA na safari yake ilianza vipi? Kufahamu yote hayo na mengine mengi ungana na Flora Nducha wa UN News Kiswahili aliyeketi na kuzungumza naye katika makala hii
Tanzania imesema inaunga mkono mshikamano wa kimataifa wa kutokomeza Ukimwi duniani, kauli iliyotolewa leo na Rais wa taifa hilo Samia Suluhu Hassan wakati akihutubia mkutano wa ngazi ya juu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu UKIMWI ulioanza leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kwa njia ya mtandao na ukumbini.
Akihiiitmisha ziara ya siku mbili nchini Burundi, Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, Filippo Grandi, amepongeza juhudi zilizofanywa kusaidia wakimbizi kupata suluhu ya muda mrefu katika taifa hilo ambalo ni kiini cha ukanda wa Maziwa Makuu.
Ikiwa kesho Aprili 14 ni siku ya ugonjwa wa Chagas, shirika la kimataifa la kufanikisha uwepo wa tiba nafuu duniani, Unitaid linaloratibiwa na shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO, limesema uwepo wa Covid-19 umefanya hali kuwa mbaya zaidi kwa hali ambayo tayari ilikuwa mbaya kutokana na ugonjwa wa Chagas.
Serikali ya Kenya inaendelea na kampeni ya chanjo dhidi ya corona au COVID-19 baada ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kupata na kusafirisha dozi zaidi ya milioni moja hadi Nairobi kupitia mkakati wa kimataifa wa upatikanaji wa chanjo COVAX.
Kikosi cha 7 cha Tanzania, TANZBATT_7 kwenye kikosi maalum cha kujibu mashambulizi, FIB cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO kimetamatisha jukumu lake rasmi na kukabidhi bendera kwa kikosi cha 8 au TANZBATT_8. Shuhuda wetu kutoka Beni, jimboni Kivu Kaskazini ni Luteni Issa Mwakalambo, afisa habari wa TANZBATT_7.