GBV Taarifa, programu tumishi ya kukabili ukatili wa kijinsia Tanzania
Tanzania shirika la kiraia linalohusika na masuala ya msaada wa sheria na maendeleo kwa wanawake, WiLDAF kwa kushirikiana na kampuni ya teknolojia, Dephics wametengeneza programu tumishi iitwayo GBV Taarifa inayowezesha mtu kutoa taarifa za ukatili wa kijinsia kupitia simu ya kiganjani.