Uganda yapitisha amri ya kutotembea usiku kudhibiti COVID-19
Uganda imefuata nyayo ya baadhi ya nchi duniani ya kupitisha amri ya kutotembea usiku kama mojawapo ya njia za kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa virusi vya Corona, au COVID-19, sanjari na kufunga mipaka yake na kupiga marufuku usafiri wa magari binafsi.