Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Mahojiano

UN News/Assumpta Massoi

Elimu ni mkombozi kwa msichana wa kimasai- Mamasita

Mkutano wa 62 wa Kamisheni ya Hali ya wanawake duniani, CSW62 umeanza makao makuu ya Umoja wa Mataifa, kubwa zaidi linaloangaziwa ni wanawake na wasichana wa vijiji. Wawakilishi wa mashirika ya kiraia wamefika na miongoni mwao ni Maria Mamasita kutoka Monduli mkoa wa Arusha nchini Tanzania.

Sauti
2'8"

Liberia ni mfano kwa nchi zingine zenye migogoro:Opande

Nchi nyingine za Kiafrika zilizo katika vita vya wenyewe kwa wenyewe ziige mfano wa Liberia na kumaliza mizozo ili kunusuru raia wake. Ushauri huo umetolewa na Jenerali mstaafu Daniel Opande aliyekuwa kamanda wa kwanza wa kikosi cha kulinda amani nchini Liberia. Alipozungumza na Zipporah Musau wa idara ya mawasiliano ya umma ya umoja wa Mataifa jenerali msattafu Opande asisitiza hata hivyo haikuwa kazi rahisi kufikia muafaka, kuketi pamoja kujadiliana na kudumisha amani ambayo sasa Liberia inajivunia.

Sauti
3'5"
Sarah Opendi

Bidhaa za tumbaku lazima zidhibitiwe

Bidhaa za tumbaku zinasababisha madhara mengi sana hususani kiafya. Shirika la afya duniani WHO sasa linataka kila nchi mwanachaka kuchukua hatua madhubuti kudhibiti hali hiyo kwa kuweka sheria na kuzitekeleza.

Sauti
2'28"