Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Mahojiano

Jane John (TBC-Tanzania)

Radio haifi ng'o- Jane John

Ujumbe wa siku ya radio duniani mwaka huu wa 2018 ni Radio na Michezo! Umoja wa Mataifa unataka chombo hicho adhimu kitumike kusaidia watu kuchanua na kuonyesha uwezo wao wote. Miongoni mwa watu ambao radio imeweza kuibua stadi zao ni Jane John, mtangazaji wa kike wa habari za michezo katika shirika la utangazaji nchini Tanzania, TBC. Assumpta Massoi alizungumza na Jane kwa njia ya simu kutoka Dar es salaam, Tanzania na kuanza kwa kumuuliza manufaa ya radio!

Sauti
5'10"
UNICEF/Catherine Ntabadde

Mangariba wadondosha nyembe zao Tanzania, wanaume nao wafungua masikio

Nchini Tanzania harakati za shirika la idadi ya watu duniani, UNFPA zimesaidia kuepusha wanawake na watoto wa kike siyo tu dhidi ya mila hatarishi ya ukeketaji au FGM, bali pia zimesaidia kubadili mtazamo wa wanaume kuhusu kuoa wanawake ambao hawajakeketwa. Ali Haji Hamad, afisa wa jinsia kwenye ofisi hiyo amezungumza na Assumpta Massoi kwa idhaa hii.

Sauti
6'15"