Bado haki za mtoto zinasiginwa, miaka 34 tangu CRC- UNICEF
- Mkataba umepitishwa 1989 lakini hali bado tete
- Haki zinapondwaponda kuanzia kuishi hadi kulindwa
- Ni maombolezo badala ya sherehe
Visa vya kutisha vya ukatili dhidi ya watoto hususan waliofurushwa makwao maeneo mbalimbali duniani vimesababisha viongozi waandamizi wa Umoja wa Mataifa kurejelea wito wao wa ulinzi wa watoto na kuhakikisha wakati wowote ule haki zao zinalindwa kwa mujib uwa sheria ya kimataifa, na wakati huo huo watendao uhalifu huo wasikwepe sheria.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amekaribisha maelewano yaliyofikiwa jana kati ya Umoja wa Mataifa na serikali ya Syria ya kuendelea kutumia kwa miezi sita ijayo mpaka wa Bab al-Hawa kufikisha misaada ya kibinadamu inayohitajika zaidi kwa mamilioni ya watu kaskazini-magharibi mwa Syria.
Baada ya jana Jumanne nia ya Baraza la Usalama kupitisha azimio ambalo ningeruhusu uvushaji misaada ya kibinadamu katika kivuko cha Bab al-Hawa kwenye mpaka wa Syria na Uturuki kaskazini-magharibi mwa Syria ili ikaokoe maisha ya wananchi wa nchi hiyo ambao wamekuwa kwenye zaidi ya miaka 12 ya vita kukwama kutokana na Urusi kupiga kura ya turufu kulipinga azimio hilo lingerefusha operesheni hiyo kwa miezi tisa mbele baada ya kufikia ukomo juzi tarehe 10 Julai, hofu sasa ni kuwa matokeo yake yatakuwa maumivu zaidi kwa wananchi wa Syria.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesikitishwa kwa kuona kwamba Baraza la Usalama halikuweza kufikia makubaliano leo kuhusu kurefusha idhini kwa operesheni za Umoja wa Mataifa za uvushaji wa misaada ya kibinadamu mpakani Uturuki kuingia nchini Syria.
Kwa zaidi ya muongo mmoja, watu wa Syria hawajaona chochote isipokuwa kifo, uharibifu na kukata tamaa. Watu nusu milioni wamefariki katika mzozo wa Syria. Asilimia 90 ya Wasyria wanaishi chini ya mstari wa umaskini. Mamilioni ya watu wanahitaji msaada wa kibinadamu. Na mnamo Februari mwaka huu, Wasyria pia walipata tetemeko kubwa la ardhi, ambalo lilizidisha hali yao mbaya.
Katika kambi ya wakimbizi ya Za’atari iliyoko nchini Jordan, roho ya ubunifu ya mtu mmoja na dhamira yake isiyoyumba imebadilisha vitu mbalimbali vinavyotupwa na kuonekana havifai tena kuwa nyenzo muhimu za urembo.
Leo ni miaka 12 kamili tangu machafuko yalipozuka Syria na kusababisha vita inayoendelea tangu mwaka 2011 iliyosambaratisha nchi hiyo na mamilioni ya raia wake. Maelfu wamepoteza maisha, mamilioni wamekuwa wakimbizi ndani na nje ya nchi yao na majanga mengine ya kila uchao yanazidi kuwaondolea matumaini raia wa taifa hilo la Mashariki ya Kati.
Ripoti mpya iliyotolewa leo na tume ya Umoja wa Mataifa ya uchunguzi nchini Syria inasema pande zote katika mzozo unaondelea nchini humo zimetekeleza ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na ukatili katika miezi ya kuelekea tetemeko kubwa la ardhi kuwahi kushuhuduwa kwa zaidi ya karne katika ukanda huo, na kuendeleza muongo ulioghubikwa na mwenendo wa kushindwa kuwalinda raia wa Syria.
Watoto milioni 3.7 ambao walinusurika na matetemeko ya ardhi ya tarehe 6 Februari mwaka huu katika maeneo yaliyoathirika nchini Syria wanakabiliwa na ongezeko la vitisho kadhaa vya zahma kubwa, ameonya leo Mkurugenzi mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF, Catherine Russell akihitimisha ziara yake ya siku mbili nchini humo.