Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Mashariki ya Kati

Mtoto mwenye umri wa miaka 3 anaendelea kupona baada ya kukatwa mguu wake kufuatia shambulizi la moja kwa moja la kombora nyumbani kwake katika mji wa Nuseirat katikati mwa Ukanda wa Gaza.
© UNICEF/Abed Zaqout

Mapigano Gaza sasa yanasambaa hospitali, hakuna njia ya kuingia wala kutoka: UN

Wakati mapigano makali  yakiendelea huko Gaza leo asubuhi ikiwa ni pamoja na mashambulizi yaliyoripotiwa dhidi ya hospitali katika mji wa kusini wa Khan Younis, wahudumu wa misaada wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa walionyesha wasiwasi mkubwa kwa wagonjwa na watu wengine wanaosaka matibabu ambao wamejikuta katikati ya mapigano hayo bila njia ya kuingia wala kutoka.

Mashambulizi ya anga yaharibu majengo katika Ukanda wa Gaza. (Maktaba)
© UNRWA/Ashraf Amra

Raia 25,000 wamepoteza maisha katika vita Gaza na mahitaji ya kibinadamu yanazidi kuongezeka: UN

Mashambulizi makubwa ya mabomu yanayofanywa na Israel Gaza yameendelea tena leo sanjari na maroketi yanayovurumushwa na makundi yenye silaha ya Kipalestina kuelekea Israel, wakati wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wakiripoti kuuawa kwa watu zaidi ya 25,000 Gaza tangu kuanza kwa machafuko hayo mapya Oktoba 7 mwaka jana na mahitaji ya kibinadamu yakiongezeka kila uchao.

Sauti
2'22"
Msichana mdogo amelazwa katika hospitali ya Al-Quds huko Gaza.
© UNICEF/Eyad El Baba

Hali ya Gaza ni zahma juu ya zahma: Mashirika ya UN

Mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa leo yameeielezea hali inayoendelea Gaza siku 105 baada ya kuzuka vita mpya baina ya wapiganaji wa Hamas na vikosi vya Israel, kuwa ni zahma juu ya zahma. Watu zaidi ya milioni 1.7 wametawanywa huku hofu ya milipuko ya magonjwa, janga la njaa na vifo zaidi likitawala.

Sauti
2'
Mvulana mwenye umri wa miaka 10 anachungulia tundu kwenye ukuta wa nyumba yake lililosababishwa na shambulio la anga huko Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza.
© UNICEF/Eyad El Baba

Vikwazo vya misaada Gaza vinaendelea kuchelewesha huduma muhimu: UN

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yamerejea kupaza sauti kuhusu misaada muhimu ya kibinadamu kuendelea kuruhusiwa kuingia ukanda wa Gaza, lile la kuratibu Misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura OCHA likisema kwa mara ya kwanza dawa kwa ajili ya mateka wa Israel zimeripotiwa kuruhusiwa kuingia leo sanjari na msaada kwa ajili ya Wapalestina kwa makubaliano maalum yaliyowezeshwa na serikali za Qatar na Ufaransa.

Watoto wakisubiri kugawiwa chakula huko Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza.
© UNICEF/Abed Zagout

Siku 100 za mzozo: Hatuwezi kuruhusu yanayotokea Gaza kuendelea, wala kutokea Lebanon - Guterres

Siku 100 tangu kuanza kwa mzozo wa Israel na Palestina, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres leo Januari 15 akizungumza na wanahabari jijini New York Manreakni ametaka "kuachiliwa mara moja na bila masharti kwa mateka wote. "Pia akiongeza kusema mashambulizi dhidi ya Gaza yaliyotekelezwa na vikosi vya Israeli katika siku hizi 100 yamesababisha uharibifu mkubwa na viwango vya mauaji ya raia kwa kiwango ambacho hakijawahi kutokea katika miaka ya uongozi wake kama Katibu Mkuu."