Kushamiri kwa mapigano Gaza kwamtia hofu Guterres
- Israeli upande mmoja, Hamas na makundi mengine upande mwingine
- Jeshi la Israeli lashambulia ardhini
- Makombora ya angani yaelekezwa Israeli kutoka Gaza
Huku mzozo wa Israel na Palestina ukiwa katika wiki yake ya nne, wahudumu wa misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa leo wameonya kuhusu shinikizo linaloongezeka kwenye hospitali za kaskazini mwa Gaza ambako wamesalia wagonjwa na wahudumu wa afya, huku kukiwa na ripoti za kuongezeka kwa operesheni za ardhini za jeshi la Israel.
Mashirika ya misaada yameonya hii leo kwamba utaratibu wa kiraia unaanza kuvunjika huko Gaza baada ya maelfu ya watu waliokata tamaa kuvamia maghala yanayosimamiwa na Umoja wa Mataifa na vituo vingine vya usambazaji wa misaada katika eneo lililoharibiwa, wakichukua unga wa ngano, vifaa vya usafi na bidhaa nyingine muhimu za kujiokoa.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ameanza ziara yake rasmi nchini Nepal kwa kutoa salamu za rambirambi kwa familia za wanafunzi 10 wa Nepal waliouawa katika mashambulizi ya kigaidi yaliyofanywa na Hamas nchini Israel, na kwa mara nyingine tena kutoa wito wa kulindwa kwa raia wote huko Gaza akisema, “hali inakua ya kukatisha tamaa kila saa.”
Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk amezikumbusha pande zote katika mgogoro unaoendelea Mashariki ya Kati kuzingati wajibu wao chini ya sheria ya kimataifa ya kibinadamu na sheria ya kimataifa ya haki za binadamu.
Wakati wa usiku wa mashambulizi makali ya mabomu na uvamizi wa ardhini ukifanyika huko Gaza, Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani WHO limesema ripoti za uhasama bado zinandelea, huku wafanyakazi wa afya, wagonjwa na raia wakikumbwa na kukatika kwa mawasiliano na kukatika kwa umeme.
Licha ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hapo jana kupitisha azimio la kutaka mshambulizi kusitishwa kwa sababu za kibinadamu huko Ukanda wa Gaza, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameeleza kusikitishwa kwake na ongezeko lisilo la kifani la mashambulizi.
Hali mbaya inayowakabili mamia kwa maelfu ya Wapalestina huko Gaza inaweza kuwa mbaya zaidi, kutokana na uhaba mkubwa wa mafuta ambao unatishia kusimamisha chakula na shughuli zingine za kibinadamu.
Mratibu wa mwasuala ya kibinada wa Umoja wa Mataifa kwenye eneo linalokaliwa la Palestina Lynn Hastings amesema Gaza imepoteza mawasiliano na Dunia wakati kukiwa na tarifa za kushamiri kwa mashambulizi ya mabonu.