UN yakaribisha muafaka wa usitishaji mapigano na kuachilia mateka Gaza
Muafaka uliofikiwa jana jioni wa kuwaachilia mateka waliochukuliwa wakati wa shambulizi la Hamas huko Israel Kusini Oktoba 7 umekaribishwa na Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ambaye amesema Umoja huo uko tayari kutumia hatua hiyo njema kwa ajili ya masuala ya kibinadamu.