Hatua za mapema dhidi ya hali ya hewa zina manufaa
Kupitia mipango ya mapema, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na wadau wake wanapunguza athari za hali mbaya ya hewa katika nchi zinazokabiliana na njaa.
Kupitia mipango ya mapema, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na wadau wake wanapunguza athari za hali mbaya ya hewa katika nchi zinazokabiliana na njaa.
Wiki za mvua kubwa na mafuriko huko Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika kumechuochea ukimbizi amapo mamia ya maelfu ya watu wamefurushwa makwao huko Burundi, Kenya, Rwanda, Somalia na Tanzania ambapo Umoja wa Mataifa unasema hadi tarehe 3 mwezi huu wa Mei, jumla ya 637,000 wameathiriwa, 234,000 kati yao hao wamelazimika kukimbia makwao.
Maelfu ya watu, wakiwa ni pamoja na wakimbizi, wanaendelea kukumbwa na mvua kubwa kufuatia mvua za El Niño na mafuriko makubwa yanayozikumba sehemu nyingi za Afrika Mashariki. Umoja wa Mataifa unataja wakimbizi walioathiriwa ni wale walioko Tanzania, Somalia na Burundi.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema amesikitishwa sana kusikia mamia ya watu wameopoteza maisha na wengine wengi kuathiriwa na mafuriko makubwa katika nchi za Burundi, Kenya, Somalia na Tanzania na maeneo mengine ya Afrika Mashariki.
Nchini Burundi shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limechukua hatua kuhakikisha watoto wakimbizi wanaorejea nchini humo wanaweza kuendelea na elimu bila uoga na jakamoyo hasa pale wanapokumbana na vizuizi vya tofauti ya lugha waliyotumia ukimbizini na ile inayotumika nyumbani walikorejea.