Neno la Wiki - Hayati na Marehemu tofauti ni ipi?
Hii leo katika Neno la Wiki, Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi kutoka Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA, anatofautisha maana ya maneno 'Hayati' na 'Marehemu'. Katika uchambuzi wake wa maneno hayo yenye etimolojia ya kiarabu, anafafanua tofauti katika matumizi. Karibu!