Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

© Education Cannot Wait/Daniel Beloumou

Uwekezaji katika elimu kwa watoto utawasaidia kupambana na mabadiliko ya tabianchi

Pazia la mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP28 likitarajiwa kufungwa hapo kesho huko Dubai Falme za kiarabu tunaangazia suala la jinsi mabadiliko ya tabianchi yanavyoathiri watoto hususani katika suala la Afya na kwenye elimu. 

Tarehe 08 Desemba ratiba ya COP28 ilijikita mahususi kujadili masuala ya vijana na watoto. Mashirika mbalimbali yalitoa takwimu zinazohusiana na madhara ya mabadiliko ya tabianchi kwa watoto na vijana moja wao ni Mfuko wa kimataifa wa elimu haiwezi kusubiri ECW. 

Sauti
3'13"
UN News

Kituo cha afya cha Mtofaani kwa hisani ya Milele Zanzibar Foundation utekelezaji wa SDG 3

Shirika lisilo la kiserikali la Milele Zanzibar Foundation la Zanzibar Tanzania ambalo limejipambanua kujikita na utekelezaji wa malengo 12 kati ya malengo 17 ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo Endelevu, limetekeleza lengo namba 3 la Afya Bora na Ustawi kwa kujenga kituo cha afya katika Shehia ya Michikichini, Unguja. Hamad Rashid wa redio washirika wetu Mviwata FM ya Morogoro - Tanzania amefika visiwani humo na kutuandalia makala hii.

Sauti
4'25"
UN News

Siku ya ulemavu duniani: Kauli kutoka kwa mchezesha muziki mwenye ulemavu wa kutoona

Siku ya watu wenye ulemavu duniani iliadhimishwa jana desemba 3 ikiwa na maudhui Ushirikiano katika hatua ya kuokoa na kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu, (SDGs) kwa  pamoja na watu wenye ulemavu, na leo inakupeleka nchini Kenya kummulika mchezeshaji muziki au DJ mwenye ulemavu wa kutoona John Ndichu al maarufu, DJ NdichiKings. Pamela Awuori wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa amezungumza naye akiwa eneo la Ruiru, Kaunti ya Kiambu. 

Sauti
3'14"
UNAIDS

SHDEPHA+ yatekeleza kwa vitendo kauli ya UNAIDS ya jamii zishike hatamu kutokomeza Ukimwi

Leo ni siku ya Ukimwi duniani takwimu zikionesha kupungua sio tu kwa asilimia 70 ya vifo ikilinganishwa na mwaka 2004, idadi ilipokuwa kiwango cha juu zaidi duniani, bali pia maambukizi mapya ikilinganishwa na miaka ya 1980. Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la UNAIDS linasema miongoni mwa sababu za kupungua ni ushiriki wa jamii, yaani jamii kushika hatamu za vita dhidi ya Ukimwi.

Sauti
5'22"
UN News/ Assumpta Massoi

Simulizi: Jina langu ni Selemani lakini nilikuwa naitwa Selina

Wakati kila kona ya dunia kwa sasa ikiadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, harakati hizo miaka ya 1987 hazikuwa rahisi kueleweka ndani ya baadhi ya jamii kwani mila na destuli ambazo nyingine zilijikita katika mfumo dume ndizo zilizokuwa zimetamalaki. Lakini wanaharakati walitumia mbinu mbalimbali hata kubadili majina ili waweze kufanya kazi ya kubadilisha mitazamo ndani ya jamii.

Sauti
3'18"
UN News/ Byobe Malenga.

Misaada tunapata lakini tunachohitaji zaidi ni amani- Mkimbizi wa ndani DRC

Hivi karibuni tulinukuu mashirika ya Umoja wa Mataifa, lile la kuhudumia wakimbizi UNHCR na lile la kuhudumia watoto UNICEF yakielezea wasiwasi wao mkubwa juu ya kushamiri hivi karibuni kwa mzozo wa kibinadamu mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC. Mapigano makali kati ya jeshi la serikali na vikundi vilivyojihami katika muda wa wiki sita tu yamesababisha watu 450,000 kukimbia makwao kutoka maeneo ya Rutshuru na Masisi katika jimbo la Kivu Kaskazini.

Sauti
3'19"
© UNICEF/Zahara Abdul

Waepushe watoto wachanga na bidhaa za viwandani – WHO/UNICEF

Kwa mujibu wa mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa lile la Afya Ulimwenguni (WHO) na la Kuhudumia Watoto (UNICEF), tabia za ulishaji wa vyakula visivyo salama kiafya kwa watoto wadogo na wachanga lazima ziepukwe kwasababu zinachangia kuongezeka uzito usio salama kiafya, na vyakula hivyo vinaweza kuchukua nafasi ya vyakula vyenye virutubishi muhimu kwa watoto.

Sauti
3'37"
© UNICEF/Paul Kidero

Mataifa yaongeze kasi ya mabadiliko katika kuhakikisha upatikanaji wa choo safi na salama

Wakati hapo jana Novemba 19 dunia imeadhimisha Siku ya choo Duniani. maudhui yaliyobeba siku hiyo ni ‘Kuongeza kasi ya mabadiliko’. Kampeni hii inazingatia athari za janga la usafi wa mazingira ambalo huwa chanzo cha magonjwa mengi hasa ya kuambukiza. Kwa mujibu wa takwimu za shirika la afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO watu bilioni 3.6 karibu nusu ya watu wote duniani hawana huduma za msingi za usafi na milioni 494 miongoni mwao wanajisaidia haja kubwa katika maeneo ya wazi kwa kukosa huduma ya choo wengi wakiwa ni kutoka katika nchi masikini.

Sauti
4'33"
UN News/Daniel Dickinson

Juhudi za pamoja zimesaidia kudhibiti kipindupindu Zanzibar: WHO

Mtazamo wa kujumuisha sekta mbalimbali na kuishirikisha kikamilifu jamii imekuwa chachu kubwa ya kudhibiti milipuko ya ugonjwa wa kipindupindu iliyokuwa ikikiandama kisiwa cha Zanzibar kwa muda mrefu limesema shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO. Mtazamo huo ambao unaunganisha kampeni za uelimishaji kwa jamii kupitia ufadhili wa muungano wa chanjo duniani GAVI na msaada wa wadau mbalimbali likiwemo shirika la WHO imekisaidia kisiwa hicho kutokuwa na mgonjwa hata mmoja wa kipindupindu katika miaka mitano iliyopita. Ungana na Flora Nducha kwa makala hii kwa kina.

Sauti
3'45"