Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Misaada tunapata lakini tunachohitaji zaidi ni amani- Mkimbizi wa ndani DRC

Misaada tunapata lakini tunachohitaji zaidi ni amani- Mkimbizi wa ndani DRC

Pakua

Hivi karibuni tulinukuu mashirika ya Umoja wa Mataifa, lile la kuhudumia wakimbizi UNHCR na lile la kuhudumia watoto UNICEF yakielezea wasiwasi wao mkubwa juu ya kushamiri hivi karibuni kwa mzozo wa kibinadamu mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC. Mapigano makali kati ya jeshi la serikali na vikundi vilivyojihami katika muda wa wiki sita tu yamesababisha watu 450,000 kukimbia makwao kutoka maeneo ya Rutshuru na Masisi katika jimbo la Kivu Kaskazini. Evarist Mapesa wa Idhaa hii ameamua kufuatilia hao waliong’olewa kwenye makazi yao kusikia kile walichopitia na madhila gani yanawakumba. Ukisikia mhusika wakisema mumwezi anamaanisha mwezi, mnane ni nane na saa kenda ni saa tisa. Kwako Evarist.

Audio Credit
Pamela Awuori/Evarist Mapesa
Audio Duration
3'19"
Photo Credit
UN News/ Byobe Malenga.