Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

wiki ya chanjo kimataifa yaadhimishwa, UNICEF yatoa ujumbe.

wiki ya chanjo kimataifa yaadhimishwa, UNICEF yatoa ujumbe.

Pakua

Ikiwa maadhimisho ya wiki ya chanjo duniani yameanza leo, siku hii hutoa fursa kwa Shirika la Afya duniani WHO na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudiumia watoto duniani UNICEF kusisitiza umuhimu wa chanjo ili kuzuia magonjwa hatarishi.

Kwa mujibu wa UNICEF, watoto milioni 22 kote duniani hawajakamilisha ratiba nzima ya chanjo, hali inayosababisha zaidi ya watoto milioni 1.5 kufariki dunia kila mwaka kutokana na magonjwa hatari yanayozuiliwa kwa chanjo. Robert Kazaala afisa wa UNICEF mjini Geneva na  katika mahojiano maalum na Grace Kaneiya wa Idhaa hii anaanza kwa kueleza umuhimu wa chanjo katika kuzuia magonjwa

(SAUTI MAHOJINAO)