Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ugonjwa wa Kifua Kikuu waangaziwa nchini Kenya

Ugonjwa wa Kifua Kikuu waangaziwa nchini Kenya

Pakua

Machi 24 ni siku ya kifua kikuu duniani. Siku hii imetengwa kwa ajili ya kuhamashisha na kuleta uelewa kuhusu mzigo wa kifua kikuu na jinsi ya kukabiliana na ugonjwa huu. Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Fikia watu hao milioni 3”. Shirika la afya duniani WHO linasema kwamba ijapokuwa ugonjwa wa kifua kikuu unatiba lakini theluthi moja ya watu milioni tisa ambao huugua ugonjwa huo hawapati tiba. Watu hao milioni tatu wanaishi katika jamii masikini ama watu walio hatarini au watu walio pembezoni kwa mfano wahamiaji, wakimbizi na wakimbizi wa ndani, wafungwa na watu wa asili, au watu wanaotumia madawa ya kulevya.

Kumepigwa hatua katika kupunguza viwango vya kifua kikuu na vifo kutokana na kifua kikuu vimepungua kwa asilimia 45% tangu 1990. Hii imechangiwa na Vifaa vipya na aina mpya ya madawa. Ijapokuwa hatua zimepigwa mzigo huu ni mzito na changamoto zipo hususan katika nchi zinazoendelea. Basi ungana na Salim Chiro kutoka radio washirika pwani FM nchniKenyaili kupata hali ilivyo kuhusu kifua kikuu.