Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

31 JULAI 2023

Hii leo jaridani mwenyeji wako ni Leah Mushi akimulika masuala ya afya hususan mafanikio ya será za kudhibiti uvutaji sigara na tumbaku; elimu kwa watoto waliokosa fursa huko Kenya; nishati salama nchini Tanzania na ujumbe wa Romeo George mwanaharakati wa SDGs.

Sauti
12'44"

27 JULAI 2023

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo Jacqueline Woiso, Mkurugenzi Mwendeshaji wa Multichoice Tanzania anafafanua ni malengo yapi ya Maendeleo Endelevu yaliyoipa Multichoice Tanzania Ushindi wa Tuzo ya UN Global Compact. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo ripoti ya hali ya hewa, jaribio la kutaka kutwaa madaraka kijeshi nchini Niger na uhifadhi wa bioanuwai barani Afrika. Katika kujifunza lugha ya Kiswahili tunakuletea maana ya neno “NDOFYA". 

Audio Duration
10'

26 JULAI 2023

Hii leo jaridani tunaangazia ripoti ya UNESCO kuhusu teknolojia na pia afya ya wanawake wajawazito nchini Sudan. Makala tunakupeleka nchini Australia na mashinani Roma nchini Italia, kulikoni? 

Sauti
13'7"

25 JULAI 2023

Hii leo jaridani mada kwa kina ambapo wakimbizi kutoka nchini Rwanda na Burundi wanaopata hifadhi katika nchi Jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, wamepata matumaini mapya ya maisha baada ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na shirika lisilo la kiserikali ya AIDES kuwawezesha kuanzisha mradi wa kazi za Sanaa ambao unawasidia kujikimu kimaisha pamoja na familia zao. Ashinani tutaelekea Bahari ya Shamu au Red Sea, kulikoni? 

Sauti
11'55"

24 JULAI 2023

Hii leo jaridani mwenyeji wako ni Leah Mushi akimulika mkutano wa mifumo ya chakula ulioanza leo Roma, Italia; Kauli ya mshiriki kutoka Tanzania kwenye mkutano uliomalizika hivi karibuni hapa makao makuu ya UN; Makala anabisha hodi Rwanda ilhali mashinani anakupeleka Tunisia.

Sauti
11'55"

20 JULAI 2023

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo Jukwaa la ngazi ya juu la kisiasa kuhusu malengo ya maendeleo endelevu lijulikanalo kama HLPF linafikia tamati hii leo hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York-Marekani. Wawakilishi wa nchi na serikali, wanasayansi, wanazuoni, mashirika ya umoja wa Mataifa, asasi mbalimbali na vijana wamekutana kuanzia tarehe 10 Julai kujadili hatua za kuchukua ili kuhakikisha malengo hayo muhimu ya maendeleo yanatimizwa ifikapo mwaka 2030.

Sauti
13'39"

19 JULAI 2023

Hii leo jaridani tunaangazia jukwaa la ngazi ya juu la kisiasa la Umoja wa Mataifa  kuhusu malengo ya maendeleo endelevu kwa kifupi HLPF ambalo linakaribia kufikia ukingoni na pia ukame nchini Kenya. Makala tunasalia hapa hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa na mashinani tunakupeleka nchini Yemen, kulikoni? 

Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Sauti
11'25"

18 JULAI 2023

Hii leo Jumanne ya Julai 18, siku ya kimataifa ya Mandela mwenyeji wako ni Leah Mushi akikuletea Habari kwa Ufupi zikisomwa na Anold Kayanda, kisha anakupeleka Iringa nchini Tanzania kumulika harakati za shirika la kiraia la Afya Plus za kusongesha lengo namba 6 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs kuhusu maji safi na kujisafi kupitia maabara za hedhi salama, mradi unaofadhiliwa na Mfuko wa Malala. Kisha mashinani anakurejesha hapa makao makuu ya UN kusikia wito wa kwamba kufanikisha SDGs lazima uwe na moyo kama wa mama. Karibu!

Sauti
13'20"

17 JULAI 2023

Hii leo katika jarida la Habar iza UN, mwenyeji wako Leah Mushi anamulika haki za binadamu za watu wa jamii ya asili, haki ya elimu kwa watoto wakimbizi, saratani ya shingo ya kizazi na hatimaye jinsi kampeni ya boma kwa boma inasongesha utoaji chanjo kwa jamii ya wamasai nchini Tanzania.

Sauti
11'11"