Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

27 JULAI 2023

27 JULAI 2023

Pakua

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo Jacqueline Woiso, Mkurugenzi Mwendeshaji wa Multichoice Tanzania anafafanua ni malengo yapi ya Maendeleo Endelevu yaliyoipa Multichoice Tanzania Ushindi wa Tuzo ya UN Global Compact. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo ripoti ya hali ya hewa, jaribio la kutaka kutwaa madaraka kijeshi nchini Niger na uhifadhi wa bioanuwai barani Afrika. Katika kujifunza lugha ya Kiswahili tunakuletea maana ya neno “NDOFYA". 

  1. Kufuatia ripoti iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya hewa WMO kwa kushirikiana na lile la Kamisheni ya Muungano wa Ulaya ambayo imethibitisha kuwa mwezi huu wa Julai utavunja rekodi ya dunia ya kuwa na joto kali ulimwenguni kote,  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema takwimu hizi mpya ni uthibitisho kuwa ubinadamu umeketi katika kiti cha moto na kwamba lazima hatua zichukuliwe haraka.
  2. Tukitoka Marekani tuelekee Geneva Uswisi ambako Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk ameshtushwa, amehuzunishwa na kulaani vikali jaribio la kutaka kutwaa madaraka kijeshi nchini Niger lililofanyika hapo jana.
  3. Na Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO limekaribisha mchango wa zaidi ya dola milioni 27 uliotolewa na Muungano wa Ulaya kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya uhifadhi wa bioanuwai barani Afrika.
  4. Na Leo katika kujifunza lugha ya Kiswahili nampisha Dkt. Mwanahija Ally Juma Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Zanzibar, BAKIZA akitufafanualia maana ya neno “NDOFYA".

Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
10'