Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

UNICEF/ Ethiopia/2018/Mersha

Mtoto wa kiume atumbia mbinu kuepusha mtoto wa kike kuozwa

Nchini Ethiopia ambako asilimia 40 ya wasichana wanaolewa kabla ya kufikia umri wa miaka 18, msichana Tsigist Wudu Chekol ilikuwa kidogo tu awe miongoni mwa hao lakini akaponea chupuchupu na sasa ni mwanachama wa kikundi cha wasichana katika shule anayosoma, kinachopambana kuhakikisha katika jamii hakuna mtoto anayeolewa kabla ya wakati. Ahimidiwe Olotu na maelezo zaidi.

Audio Duration
1'48"
TANZBATT 7/Ibrahim Mayambua

Mauaji ya raia DRC yanachukiza, mamlaka wajibisheni wahusika- Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  Antonio Guterres amerejea wito wake wa kusitisha uhasama kimataifa na kuyataka makundi yote yenye silaha kuweka silaha hizo chini na kujiunga katika mchakato wa amani, baada ya raia zaidi ya 20 kuuawa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC. Jason Nyakundi na maelezo zaidi.

Akisistiza umuhimu wa serikali ya DRC kuchukua hatua madhubuti kushughulikia vyanzo vya mizozo Mashariki mwa nchi hiyo Katibu Mkuu amesema raia wasio na hatia hupoteza maisha kila uchao vita vinapoendelea. 

Sauti
1'26"
WFP/Jonathan Eng

NIlisaidiwa , sasa ni wakati wangu kusaidia :Liberee

Wahenga walinena ukishikwa shikamana, na ndivyo anavyofanya Liberee Kayumba ambaye ni manusura wa mauaji ya kimbari ya Rwanda dhidi ya Watutsi yaliyofanyika mwaka 1994, anasema yuko hai leo hii sababu ya msaada wa chakula wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP , ambao ulimuhamasisha baadaye kujiunga na shirika hilo kusaidia wakimbizi wa Burundi kama alivyosaidiwa. John Kibego anasimulia zaidi 

(TAARIFA YA JOHN KIBEGO) 

Sauti
2'12"
UN Photo/Herve Serefio

Buriani walindaamani wetu:MINUSCA

Umoja wa Mataifa kupitia mpango wake wa kuweka utulivu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, MINUSCA umewaaga kwa heshima  walinda amani kutoka Burundi, Bangladesh, na Cameroon ambao walipoteza maisha yao hivi karibuni wakiwa kazini. Taarifa ya Ahimidiwe Olotu inaeleza zaidi. 

(Taarifa ya Ahimidiwe Olotu) 

Sauti
2'42"
©FAO/Natalia Merkusheva

Kijana, lazima utunze vizuri kumbukumbu za biashara yako ili uaminike-Ashford Kariuki

Ashford Kariuki ni kati ya vijana ambao wamenufaika na mkopo kutoka kwa hazina ya maendeleo ya vijana nchini Kenya ambayo ilibuniwa kwa lengo la kuwainua vijana walio na ndoto za kujiajiri na kujiendeleza kimaisha. Baada ya masomo ya shule ya upili alianzisha biashara ya kuwauzia wakulima chakula cha mifugo. Mwaka uliopita alifanikiwa kupata mkopo wa lori kutoka hazina hiyo ya vijana ikiwa ni hatua kubwa katika biashara yake. Amezungumza na mwandishi wetu wa nchini Kenya, Jason Nyakundi.

Sauti
3'35"
WFP/Matteo Cosorich

Mapambano dhidi ya tabianchi, kijana Nkosi wa Zimbabwe atumia kipaji chake cha kuongea.

Nchini Zimbabwe kijana mdogo wa umri wa miaka 17 anatumia kipaji chake cha kuongea kuhamasisha mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.

Huyo ni Nkosilathi Nyathi mwenye umri wa miaka 17, mkazi wa Victoria Falls, Zimbabwe. Akitumia kipaji chake cha kuzungumza na kughani katika kueneza elimu ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi. 

Sauti
1'6"
IOM Bole Addis Ababa International Airport

Mhamiaji asimulia mazingira ya Libya yalivyokuwa tete hadi akarejea nyumbani Sudan.

Kutana na muhamiaji Mohamed Ahmed Bushara aliyekwenda kusaka maisha Libya miaka mitano iliyopita lakini hali ngumu, ubaguzi , machafuko na kuwekwa rumande vilimkatisha tamaa ya kukimbiza ndoto hiyo na akakata shauri kurejea nyumbani Sudan kushika ustaaranu mwingine kwa msaada wa shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM na Muungano wa Ulaya. 

Sauti
2'22"