Mkimbizi wa ndani nchini Yemen aliyepata ajali akiwa kazini asema hajakata tamaa
Nchini Yemen maisha ya ufukara ni dhahiri miongoni mwa wakimbizi wa ndani ambapo hata kwa wale ambao walibahatika kupata vibarua, ajali kazini imeleta madhila na machungu zaidi na kuzidi kutia mashaka mustakabli wa watoto nchini humo kama anavyosimulia Anold Kayanda
(Taarifa ya Anold Kayanda)
Upepo unavuma katika kambi ya wakimbizi ya Al Shaheed jimboni Al Mukha nchini Yemen. Abdullah Jaber anarejea kwenye kibanda chake cha mabati kisicho hata na paa, akiwa na kile kitakachokuwa mlo wa siku kwa familia yake ya mke na watoto wawili.