UNITAID yahamasisha ufadhili wa Oksijeni
Kuelekea siku ya kimataifa ya kutokomeza ugonjwa wa Nimonia duniani, shirika la Umoja wa Mataifa la kufanikisha upatikanaji wa tiba nafuu UNITAID limetoa wito kwa washirika wote kuongeza kwa kasi ufadhili katika uzalishaji wa oksijeni na kujiunga na ubia wa kampeni ya KILA PUMZI INAHESABIKA ili kuhamasisha kupunguza vifo vitokanavyo na uchafuzi wa hewa.
Leah Mushi anataarifa zaidi.