Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

© UNFPA Tanzania/Bright Warren

Taasisi ya Benjamin Mkapa yasaidia kuimarisha huduma za afya vijijini kwa kuwandaa wahudumu wa afya

Miongoni mwa taasisi hizo ni ile ya Benjamin Mkapa nchini Tanzania ambayo kwa kushirikiana na serikali ina miradi mbali mbali ya kuhakikisha wakazi wa vijini wanapata huduma ya afya na watoa huduma nao wanavutiwa kufanya kazi maeneo hayo kama anavyofafanua Dkt Ellen Mkondya Senkoro, Afisa Mtendaji Mkuu kwenye taasisi hiyo alipohojiwa mapema mwaka huu na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani.

Sauti
2'39"
UNHCR/L.Boldrini

Hatimaye manusura 116 wa ajali ya boti waruhusiwa kuteremka kutoka boti ya uokozi huko Sicily.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema manusura 116 wa ajali ya boti ya wiki iliyopita waliokuwa wakishikiliwa hadi leo Jumatano Julai 31 ndani ya boti ya ukozi ya Italia kwenye bandari ya Sicily wameruhusiwa kuteremka kutoka kwenye boti hiyo.

UNHCR inasema manusura hao walioondoka Libya kwa kutumia boti mbili waliokolewa baharini na walinzi wa doria wa Italia Julai 25 na kuhamishiwa katika boti ya walinzi wa pwani ya Bruno Gregoretti.

Sauti
1'45"
Finnish Red Cross/Maria Santto

Changamoto ya kupambana na Ebola DRC ni fedha:UNICEF

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limesema litahitaji kuongeza mara tatu bajeti yake ili kufanikisha operesheni zake kwenye majimbo ya Ituri na Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC ambayo yanakabiliwa na mlipuko wa Ebola sambamba na surua.  Assumpta Massoi na taarifa zaidi.

Sauti
1'46"
© UNICEF/UNI91025/Noorani

Kukomesha usafirishaji haramu ni jukumu la dunia nzima:UN

Usafirishaji haramu wa binadamu ni uhalifu mbaya kabisa na unagusa kila pembe ya dunia, huku waathirika wakubwa wakiwa ni wanawake, wasichana na watoto umesema leo Umoja wa Mataifa. Arnold Kayanda na ripoti kamili. 

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa leo na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya uhalifu na madawa UNODC ,katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupinga usafirishaji haramu wa binadamu, asilimia 72 ya waathirika wa uhalifu huu ni wanawake na wasichana huku idadi ya watoto waliothirika ikiongezeka mara mbili tangu mwaka 2004 hadi 2016.

Sauti
3'55"
©FAO/Christabel Clark

Magugu maji yaleta nuru kwa wakazi wa Ougadougou Burkina fasso

Ili kutatua changamoto kubwa zinazoikabili dunia hivi sasa kuanzia umaskini, mabadiliko ya tabianchi na hata majanga ya asili tunahitaji utashi, hatua zaidi na hatua zenyewe zichukuliwe sasa. Kauli hiyo imetolewa na bingwa kijana wa mwaka  2017 wa kupigania maslahi ya dunia Mariama Mamane kutoka Burkina Faso. Tupate maelezo zaidi na Jason Nyakundi

Sauti
1'49"
UN / Evan Schneider

Blogu ya Beyond the lines ni jawabu kwa vijana kuelewa SDG 16 Kenya

Mwanaharakati wa haki za binadamu kutoka Kenya ambaye pia ni afisa programu wa shirika la kiraia la Haki Afrika Wevyn Muganda amezungumzia vile ambavyo blogu yake ya Beyond the Lines inasaidia kuwezesha vijana kusoma taarifa mbalimbali bila ugumu wowote na hivyo kufanikisha leng namba 16 la maendeleo endelevu, SDGs kuhusu amani,  haki na taasisi thabiti.

Sauti
2'12"
UNICEF/Frank Dejongh

Mradi wa UNICE na kampuni kutoka Colombia ni mfano wa kuua ndege wawili kwa jiwe moja

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa ushirikiano na kampuni ya biashara ya kijamii ya Colombia Conceptos Plasticos, leo wametangaza kuzindua kiwanda cha kwanza cha aina yake ambacho kitabadilisha taka za plastiki zilizokusanywa nchini Cote d'Ivoire na kuzifanya kuwa matofali ya kawaida ya plastiki ya gharama nafuu na yanayodumu kwa muda mrefu, ambayo yatatumika kujenga vyumba vya madarasa vinavyohitajika sana katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

Sauti
2'48"