Jarida 31 Januari 2022
Miongoni mwa tuliyonayo kutoka Umoja wa Mataifa
Miongoni mwa tuliyonayo kutoka Umoja wa Mataifa
Miongoni mwa tuliyonayo hii leo
Jamii ya Maasai tarafa ya Liliondo, Wilayani Ngorongoro katika mkoa wa Arusha kaskazini mwa Tanzania waanza kuamia katika shughuli ngeni kwao, kilimo baada ya shughuli yao ya kitamaduni yaani ufugaji, kuathiriwa na mabadiliko ya tabianchi.
Mnyumbuliko wa hivi karibuni wa virusi vya Corona vinavyosababisha Covid-19, Omicron ukiwa umesambaa ulimwenguni kote, ukosefu wa usawa wa chanjo unaweka baadhi ya watu hatarini zaidi kuruhusu minyumbuliko kubadilika na kuathiri wanadamu wengine.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema walimu nchini Honduras wanaathiriwa kwa kiasi kikubwa na ghasia za magenge ya wahalifu na sasa walimu wanatambuliwa kuwa moja ya makundi yenye uwezekano mkubwa wa kulazimika kuyakimbia makazi yao.
Miongoni mwa tuliyonayo hii leo
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema walimu nchini Honduras wanaathiriwa kwa kiasi kikubwa na ghasia za magenge ya wahalifu.
Miongoni mwa tuliyonayo
Luteni Jenerali Shailesh Tinaikar raia wa India ambaye anastaafu wadhifa wake kama Kamanda wa Kikosi cha Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini, UNMISS amewashukuru askari walinda amani waliokuwa chini yake hususani wanawake ambao anasema wanafanya kazi katika m
Msimu wa upanzi wakati wa majira ya chipukizi ukiwa unakaribia huko nchiin Afghanistan, shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO limepatia wakulima mgao wa mbegu bora za ngano ili kuepusha njaa ilIyowakumba mwaka jana kutokana na kuchelewa kupanda mbegu bora wakati wa msimu wa baridi
Familia za wakimbizi wa ndani pamoja na zile zilizowakaribisha wakimbizi hao katika ukanda wa mashariki ya kati kwa sasa zinakabiliana na baridi kali kutokana na kuanguka kwa theluji wakati huu wanaishi kwenye mahema.Taarifa ya MINUSCA inayosomwa studio na Happiness Palangyo wa radio wa