Mcheza kwao hutuzwa, Kalah Jeremiah
Shirika la idadi ya watu, UNFPA limewatunukia watu ambao wanapigania usawa wa kijinsi katika jamii nchini Tanzania ambapo msanii wa Hip Hop Kalah Jeremiah amekuwa miongoni mwa watu 16 waliopata tuzo hiyo.
Shirika la idadi ya watu, UNFPA limewatunukia watu ambao wanapigania usawa wa kijinsi katika jamii nchini Tanzania ambapo msanii wa Hip Hop Kalah Jeremiah amekuwa miongoni mwa watu 16 waliopata tuzo hiyo.
Kuelekea uchaguzi wa rais na wabunge nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR tarehe 27 mwezi huu wa Desemba, shehena ya vifaa vya uchaguzi vimewasili kwenye mji mkuu wa nchi hiyo Bangui ikiwa ni msaada kutoka Afrika Kusini na walinda amani wa Umoja wa Mataifa pamoja na serikali wanashirikiana kweny
Nchini Tanzania, vijana waanzilishi wa asasi ya “They Need Us Initiative” yenye lengo la kuhamasisha vijana kushiriki katika jamii zao kuifanya dunia kuwa mahali bora pa kuishi, wametoa wito kwa wadau mbalimbali kuwaunga mkono katika mkutano wao utakaofanyika mwishoni mwa wiki ijayo.
Kutana na Sergio Chekaloff ambaye kwa zaidi ya miongo saba anaishi bila utaifa baada ya nchi tatu alizodhani kuwa ni asili yake ambazo ni Ujerumani, Urusi na Armenia zote kukataa kumtambua na sasa kwa msaada wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR anaishi Ibiza nchi
Sikiliza Jarida la Habari la Jumatano Desemba 9, 2020 na Flora Nducha
Wanawake wengi duniani, pamoja na sababu nyingine, kutokuwa huru kiuchumi kunawaweka katika hatari ya kunyanyaswa.
Tukiwa bado na siku 16 za harakati za kupinga uakatili wa kijinsia dhidi ya wanawake, leo tunamulika mwanaharakati wa haki za binadamu kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC , Francoise Sabuni Chikunda ambaye amepitia madhila yasiyoelezeka, ikiwemo kubakwa na hata familia yake kuuawa, lakini
Ukosefu wa usawa wa jinsia, ugumu wa kupata huduma na umaskini vinaripotiwa kuchochea kiwango kikubwa cha mimba za utotoni na na virusi vya Ukimwi VVU huko Homa Bay nchini Kenya.
Idadi ya watoto wa shule walioathiriwa na kufungwa kwa shule kutokana na janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19 imeongezeka kwa asilimia 38 mwezi uliopita wa Novemba, hali hiyo ikiweka mkwamo mkubwa kwenye maendeleo ya masomo na ustawi wa wanafunzi zaidi ya milioni 90 ulimwenguni, limeeleza
Sikiliza Jarida la Habari la Jumanne, Desemba 2020 kwa Habari kemkem na makala na Flora Nducha.