Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uboreshaji taaluma ya ualimu kwa ufadhili wa UNESCO Kenya

Uboreshaji taaluma ya ualimu kwa ufadhili wa UNESCO Kenya

Pakua

Mapema wiki hii nchini Kenya, kumefanyika warsha kwa ajili ya kuimarisha upatikanji wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia, OER, kwa lengo la kuimarisha elimu barani Afrika. Warsha hiyo iliendeshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni, UNESCO mjini Nairobi Kenya.

OER ni mfumo ambao unawezesha wadau mbali mbali katika sekta ya elimu kupata stadi mbali mbali kupitia vifaa hivyo vinavyopatikana bila kuhitaji leseni, iwe ni kwa mfumo wa dijitali au analojia kwani leseni inakuwa wazi kwa ajili ya kuwezesha matumizi yake bila malipo na mtu kuweza kutumia vyovyote atakavyo.

Ili kupata uelewa Zaidi wa OERni nini na lengo lake ni lipi Grace Kaneiya katika mahojiano amezungumza na washiriki wa warsha hiyo

Photo Credit
Wakati wa warsha kuhusu OER, UNESCO Kenya.(Picha:UNESCO/S.Mwanje)