Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatua za dharura zinahitajika wakati huu Malawi ikikabiliwa na Ukame mkali

Majaribio ya upandaji maharagwe yanayostahimili ukame nchini Malawi. (Maktaba)
© CIAT/Neil Palmer
Majaribio ya upandaji maharagwe yanayostahimili ukame nchini Malawi. (Maktaba)

Hatua za dharura zinahitajika wakati huu Malawi ikikabiliwa na Ukame mkali

Tabianchi na mazingira

Takriban watu milioni tisa nchini Malawi wanakumbwa na athari mbaya za mafuriko na ukame unaosababishwa na El Niñohali iliyo haribu mavuno na kupelekea ongezeko la viwango njaa na utapiamlo.

Wakizungumza wakiwa mjini Blantyre nchini Malawi, Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya Mgogoro wa Mabadiliko ya Tabianchi na El Niño Bi. Reena Ghelani, Mkurugenzi wa wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP Dkt. Menghestab Haile na Mkurugenzi la shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO nchini humo Dkt. Patrice Talla wamesisitiza umuhimu mkubwa wa msaada wa kimataifa kwa Serikali na watu kwa Malawi. 

kufuatia Rais wa Malawi kutangaza janga la kitaifa viongozi hao kwa pamoja wamefanya ziara maalum nchini humo na kukutana na wadau wa masuala ya kibinadamu na maendeleo, pamoja na maafisa wa Serikali, ikiwa ni pamoja na mamlaka ya Usimamizi wa Hatari za Maafa.

Alipokutana na washirika wa kibinadamu na maendeleo, Dk. Menghestab Haile alisema kuwa “Ni jambo la kusikitisha kuona wakulima wakiwa wamekata tamaa kutokana na ukame, ambao siyo kosa lao kwani walipanda wakitarajia mazuri lakini mvua haikutosha.” Alielezea kuwa hakutakuwa na chochote cha kuvuna na jamii hizi zitakabiliana na njaa kali kwa mwaka mwingine msaada usipoongezwa, hali ambayo inaweza kuwa mbaya zaidi kufuatia upungufu wa akiba ya chakula na kuongezeka kwa bei ya mahindi.

Kipindi hiki cha El Niño kinatokea wakati msururu wa majanga na hatari umeongezeka, na kuathiri sana maendeleo ya Malawi kwani  hapo awali, zaidi ya watu milioni 2.2 walikumbwa na kimbunga kilichoharibu miundombinu muhimu nchini humo, kilichofuatiwa  mlipuko mbaya zaidi wa kipindupindu.

Kwa upande wake Dkt. Talla kutoka FAO alieleza kuwa “Viwango na mfululizo wa gharama ya athari za mabadiliko ya tabianchi zinatoa msisitizo wa umuhimu wa kuongeza usaidizi katika kujiandaa na kupambana na mabadiliko ya tabianchi pamoja na mnepo.”

Naye Dkt Ghelani anahimiza uwekezaji katika kusaka suluhisho endelevu zinazolenga kushughulikia mizizi ya udhaifu pamoja na kuipa kipaumbele misaada ya dharura ya wakati uliopo. Vilevile amehimiza kuungwa mkono jamii za Malawi ili kujenga mustakabali wa dhabiti na usalama wa chakula.

Msaada zaidi unahitajika

Ukame umeathiri vibaya mavuno ya mahindi ya msimu huu, na kusababisha upungufu unaokadiriwa kuwa asilimia 45 ikilinganishwa na wastani wa miaka mitano. Ifikapo mwisho wa mwaka huu, inatabiriwa takriban asilimia 40 ya watu watakumbwa na njaa kali.  Aidha, takriban watu 14,000 walihamishwa kutokana na mafuriko na maporomoko ya ardhi katika sehemu ya kaskazini mwa nchi.

Ingawa Serikali ya Malawi imetoa ombi zaidi la msaada katika kupatiwa msaada kwenye mkakati wake wa umwagiliaji wa kitaifa, juhudi hizi zinakwamishwa na upungufu wa fedha kwani ni asilimia 40 tu ya fedha zilizohitajika kwa mwaka 2023 zilizopatikana.

Mwishoni mwa mwaka 2023, Mfuko Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Kukabiliana na Dharura ulitoa dola milioni 4 kusaidia watu walioathiriwa na majanga ya tabianchi na hivi karibuni ilitangaza dola milioni 13.5 za ziada kusaidia juhudi za kukabiliana na El Niño katika ukanda wa Kusini mwa Afrika. Hata hivyo bado kuna mengi zaidi yanahitaji kufanyika.