Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

‘Blue Line’ kati ya Lebanon na Israeli ni kitu gani?

Mstari wa Buluu, mpaka kati ya Lebanoni na Israeli, karibu na Mashamba ya Sheba’a yenye utajiri wa maji.
Hugh Macleod/IRIN
Mstari wa Buluu, mpaka kati ya Lebanoni na Israeli, karibu na Mashamba ya Sheba’a yenye utajiri wa maji.

‘Blue Line’ kati ya Lebanon na Israeli ni kitu gani?

Amani na Usalama

Hivi karibuni, umeibuka tena mzozo wa miaka mingi kati ya Israeli na Lebanon kwenye mpaka wao wenye kubishaniwa kati yao. 

Katika mpaka wa kaskazini mwa Israeli, kusini mwa Lebanon, mataifa haya mawili yanavutana kuhusy kipande cha ardhi mpakani ambacho kila nchi inaona kukipoteza ni sawa na kuhamisha mpaka kuingia ndani ya nchi.

Kutokana na mzozo huo, mnamo mwaka 2022, Umoja wa Mataifa kwa madhumuni ya kuthibitisha uondokaji wa majeshi ya Israeli kutoka kusini mwa Lebanoni bila ya kuathiri makubaliano ya baadaye ya mpaka kati ya nchi hizi mbili wanachama wa Umoja wa Mataifa ilichora mstari unaofahamika kimataifa kama ‘Blue Line.’

Mwaka 2021, aliyekuwa Mkuu wa Ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Lebanon, UNIFIL ambaye pia wakati huo alikuwa Kamanda wa Kikosi, Meja Jenerali Stefano Del Col alifaafanua kwa kiasi kuhusu mstari huu. 

Blue Line ni nini?

Inayoitwa The Blue Line yaani Mstari wa Buluu, unaotambaa kwa kilomita 120 kwenye mpaka wa kusini wa Lebanon, ni muhimu wa amani ya eneo hilo. Sio mpaka.

Blue Line ni ya muda tu, na walinda amani wa UNIFIL ndio walinzi wake wa muda. Wakati wowote mamlaka za Israeli au Lebanon zinapotaka kufanya shughuli zozote karibu na Blue Line, kama vile kazi za matengenezo au shughuli za usalama, UNIFIL huomba kwamba watoe taarifa ya mapema. Hii inaruhusu UNIFIL kuzishirika mamlaka za pande zote mbili, ili kupunguza hali yoyote ya kutoelewana ambayo inaweza kusababisha kuongezeka kwa mvutano. Hatimaye, ni juu ya Israeli na Lebanon kuamua njia halisi ya mpaka wa baadaye. Wakati huo huo, UNIFIL inalenga kudumisha utulivu katika mpaka huu dhaifu na kuepuka uchokozi na matukio yasiyo ya lazima ambayo yanaweza kusababisha mzozo na uwezekano wa migogoro. Mstari wa Bluu unahitaji kuheshimiwa kwa ukamilifu na wahusika. Uvukaji wowote wa Mstari wa Bluu na upande wowote unajumuisha ukiukaji wa Azimio 1701 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na UNIFIL wanashughulikia ukiukaji wote kwa njia sawa.

Mstari wa Bluu unatokana na ramani mbalimbali za kihistoria, zingine zikirudi nyuma karibu miaka 100. Mstari wa Umoja wa Mataifa uliotokana na ramani hizi mwaka wa 2000 si mara zote unaakisi kwa uwazi katika uahalisia ardhini. Kufuatia vita ya mwaka 2006, Mstari wa Buluu ulifanywa kuwa moja ya vipengele vikuu vya Azimio namba 1701 na tangu 2007, UNIFIL imefanya kazi na pande zote kuweka alama za kuonekana - "mapipa ya buluu" - kuonesha njia sahihi ya Mstari wa Buluu. Kila moja ya mapipa 272 ya buluu ambayo kwa sasa yanaashiria mstari liliwekwa tu baada ya uchunguzi wa kina na makubaliano kutoka kwa pande zote mbili. Kupitia ofisi za UNIFIL na taratibu za uunganisho na uratibu, Blue Line ni mojawapo ya maeneo machache ambayo wahusika wameendelea kujihusisha. Kila moja ya mapipa ya buluu linawakilisha makubaliano yaliyojadiliwa kwa uangalifu ambayo utulivu wa sasa katika eneo umejengwa. Hata hivyo, nusu ya urefu wa Mstari wa Buluu bado haijawekwa alama (mwaka 2021).

Vipi ukiuvuka mstari?

Ingawa eneo kubwa ni miamba, halijaachwa. Kwa upande wa Lebanon hasa, shughuli za wakulima na wanakijiji huwaleta karibu na mstari, na wakati mwingine kuvuka, Mstari wa Buluu. Kwa sababu ya ukosefu wa alama, watu na wanyama wanaweza kuvuka kutoka upande mmoja hadi mwingine bila kufahamu. Kila kivuko, hata kama bila kukusudia, ni ukiukaji wa Azimio nambari 1701, ambalo UNIFIL hulirekodi na kuripoti kwa Baraza la Usalama. Hata hivyoi, sio ukiukaji wote wa Mstari wa Buluu ni bahati mbaya. Baadhi, kama vile uvamizi unaoendelea wa Israeli wa nusu ya kaskazini ya kijiji cha Ghajar, unajulikana sana na unaendelea. Uvukaji mwingine hautabiliki - na hata wa hatari. Hatua yoyote ya upande mmoja inayofanywa na wahusika inakuwa chanzo cha mvutano mkubwa.

Hata hivyo matukio mengine mengi bila shaka yameepukwa kutokana na alama za wazi za ulipo Mstari wa Bluu. 

Lakini amani ni tete. Ingawa sasa kuna utulivu wa kadiri, hali hii inaweza kusambaratika ghafla, na watu wanaoishi kando ya Mstari wa Buluu wanajua vizuri sana. Sababu za msingi za mzozo huo hazijatoweka. Siku moja, kosa rahisi katika wakati mgumu linaweza kusababisha tetemeko hili lililofichika. 

Kinga

Makosa yanaweza kuepukwa kwa kuheshimu Mstari wa Buluu kwa ukamilifu. Kuweka alama kwa sehemu zilizobaki za Mstari wa Bluu kutasaidia kuzuia uchochezi wa bahati mbaya na usio wa lazima ambao unaweza kuzidi kuwa mzozo, ambao unaweza kusababisha mateso makubwa ya wanadamu. Bila shaka ni kwa manufaa ya kila mtu kusonga mbele kwa hili. Pande zote mbili zimeweka kando tofauti zao za kweli ili kushiriki vyema katika kuweka alama kwenye sehemu za Mstari wa Buluu hapo awali. Sasa tunahitaji kumaliza kazi. Tunahitaji kujihusisha tena juu ya suala hili na kujenga juu ya mafanikio hayo ya zamani na makubaliano ya hivi karibuni ya mfumo uliotiwa saini na wahusika.

Kufanya hivyo kutahitaji utashi wa kisiasa. Itachukua ujasiri. Na UNIFIL iko tayari kusaidia.