Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kwa nini Haiti inatoa ombi la kuanzisha ujumbe mpya wa Umoja wa Mataifa

Wahaiti wapatao 200,000, hasa katika Port-au-Prince (pichani) wamelazimika kukimbilia maeneo ya muda  kwa sababu ya ukosefu wa usalama..
© UNOCHA/Giles Clarke
Wahaiti wapatao 200,000, hasa katika Port-au-Prince (pichani) wamelazimika kukimbilia maeneo ya muda kwa sababu ya ukosefu wa usalama..

Kwa nini Haiti inatoa ombi la kuanzisha ujumbe mpya wa Umoja wa Mataifa

Amani na Usalama

Kuanzishwa kwa ujumbe wa kitaifa wa msaada wa usalama nchini Haiti kutajadiliwa wiki hii na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wakati taifa hilo la Caribbea likiendelea kukabiliwa na mzozo wa ghasia na ukosesefu wa usalama unaosababishwa na magenge ya kiharifu ambayo yamekita mizizi katika nchi hiyo.

 

Waziri mkuu wa Haiti Ariel Henry alisisitiza wito wake wa kikosi cha kimataifa katika hotuba yake aliyoitoa wakati wa mjadala wa Baraza kuula Umoja wa Mataifa September 22.

“kwa jina la wasichana na wanawake wanaobakwa kila siku, maelfu ya familia zinakimbia nyumba zao, Watoto na vijana wa Haiti wamenyimwa haki zao za kielimu na mafunzo, kwa jina la watu wote walioathiriwa na ukatili huo unaofanywa na magenge hayo ya uhalifu, naiomba jumuia ya kimataifa kuchukua hatua za Haraka”.

Waziri Mkuu wa Haiti Ariel Henry akihutubia mjadala mkuu wa kikao cha 78 cha Baraza Kuu.
UN Photo/Cia Pak
Waziri Mkuu wa Haiti Ariel Henry akihutubia mjadala mkuu wa kikao cha 78 cha Baraza Kuu.

Kwanini ujumbe wa kimataifa wa kuweka usalama ni muhimu?

Haiti inakabiriwa na ongezeko la vurugu kwa kiwango cha hali ya juu, kuanzia January mosi na September mwaka huu mauaji ya watu 3,000 yameripotiwa, huku zaidi ya watu 1,500 walitekwa nyara kwa ajili ya kupata kikombozi. Umoja wa Mataifa  unasema takribani watu 200,000 nusu yao wakiwa ni Watoto wameyakimbia makazi yao kutokana na hatari iliyopo  katika maeneo hayo.

Ukatili wa kijinsia na unyanyasaji dhidi ya wanawake umeongezeka, huku makumi ya watoto hawawezi kuhudhuria shule kutokana na ukosefu wa usalama.

Jeshi la Haiti ni dogo na lina vifaa vya kawaida tu, Jeshi Polisi nchini humo (HNP) haliwezi kukabiliana kwa ukamilifu na vurugu hizo na wanahitaji msaada wa kimataifa ili raia wa taifa hilo waweze kurejea katika maisha yao waliyozoea kuishi bila hofu, hofu, kutekwa Nyara, na kubakwa.

Nani anaunga mkono msaada wa usalama?

Kila mmoja anakubali kwamba msaada kutoka jumuiya za kimataifa unahitajika kuunga mkono jitihada za HNP ili kurejesha utulivu. 

Hadi kufikia October 2022 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alijibu ombi la waziri mkuu Henry na kuyaomba mataifa kutoa mchango wao.

Mwezi July kwenye ziara ya mji mkuu wa Haiti Port-au-Prince, Katibu mkuu alirejelea wito kwamba hatua za haraka ni muhimu.

“umakini mkubwa unahitajika kwa hali iliyopo sasa, tunatakiwa tuwaweke wahanga na raia katika vipaumbele vyetu kama tusipochukua hatua sasa, ukosefu wa utulivu na vurugu vitakuwa na athari ya kudumu kwa vizazi vya Haiti, narudia wito wangu kwa washirika kuongeza uungaji mkono kwa polisi wa kitaifa kwa njia ya ufadhili, mafunzo au vifaa”.

Suala hilo kwa mara nyingine lilikuwa kuu katika ajenda ya majadala mkuu wa kikao cha Baraza kuu la Umoja wa Mataifa, ambao ulimalizika September 26.

Katika hotuba yake, Rais wa Marekani Joe Biden alisema “watu wa Haiti hawawezi kusubiri zaidi“ na Rais wa Jamhuri ya Dominika Luis Rodolfo Corona, alitoa wito wa “kufufua azma yetu ya pamoja ya kujenga mstakabali wenye usalama, mpana, na endelevu zaidi kwa Haiti”.

Jamii za Port-au-Prince zimeweka vizuizi vya magari yaliyotelekezwa ili kupunguza hatari ya utekaji nyara na mashambulizi ya magenge.
© UNOCHA/Giles Clark
Jamii za Port-au-Prince zimeweka vizuizi vya magari yaliyotelekezwa ili kupunguza hatari ya utekaji nyara na mashambulizi ya magenge.

Kwanini imechukua muda mrefu kuanzisha operesheni hiyo?

Jambo kubwa la kusitasita daima huwa ni nchi ipi itakayojitolea kuongoza misafara ambayo inaweza kuwa ni jukumu lenye utata na hatari, ripoti za vyombo vya habari zinaonesha kwamba magenge ya wahalifu yanadhibiti karibia asilimia 80 ya mji mkuu na waziri mkuu wa Haiti alisema kulikuwa na vikundi 162 vyenye silaha na Askari 3,000 nchini kote.

Mwishoni mwa July, Kenya ilitangaza kwamba inafikiria kuongoza juhudi za kimataifa za msaada wa usalama nchini Haiti. Maafisa wa Kenya wametembelea Haiti na kufanya mazungumzo na viongozi wa nchi hiyo na eneo la Kanda, kuhusu mamlaka na wigo katika oparesheni hiyo.

Rais wa Kenya Willium Ruto aliliambia Baraza Kuu kwamba Wahaiti “wanateseka sana kutokana na urithi mkali wa utumwa, ukoloni, hujuma na kutelekezwa”, aliongeza kuwa kukabiliana na hali hiyo ni “jaribio mwisho la mshikamano wa kimataifa na hatua za Pamoja”.

Nchi za Caribbea na wanachama wa kikundi cha kikanda ikiwa ni pamoja na Jamaica, Bahamas, Antigua na Barbuda wameeleza utayari wao wakuunga mkono operesheni hiyo.

Polisi wa Kitaifa wa Haiti wanahitaji kuimarishwa ili kuweza kukabiliana na changamoto kubwa zinazowakabili, kulingana na UN.
UNDP/Borja Lopetegui Gonzalez
Polisi wa Kitaifa wa Haiti wanahitaji kuimarishwa ili kuweza kukabiliana na changamoto kubwa zinazowakabili, kulingana na UN.

Itakuwa ni oparesheni ya aina gani

Ni muhimu kutambua kwamba ujumbe wa usalama hautakuwa operasheni ya Umoja wa Mataifa, tofauti na MINUSTAH, ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Haiti uliomalizika mwaka 2017.

Waziri mkuu Henry ameomba “msaada mkubwa” wa polisi na wanajeshi ili kuunga mkono HNP, ameongeza kwamba msaada huo “hauna budi kushinda makundi ya uhalifu, kuweka upya utaratibu na kuunda mazingira ya utendaji kazi mzuri wa serikali”.

Rais Ruto wa Kenya amesema ujumbe huo ambao unaweza kujumuisha wafanyakazi 1000 wa Kenya, utakuwa “wenye rasilimali na ufanisi”.

IOM wanatoa msaada kwa jamii zilizo hatarini huko Cité Soleil, Haiti.
WFP/Theresa Piorr
IOM wanatoa msaada kwa jamii zilizo hatarini huko Cité Soleil, Haiti.

Nini Kinafuata na Umoja wa Mataifa una jukumu gani?

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kukutana ili kuandaa mfumo na kuidhinisha misafara hiyo isyokuwa ya Umoja huo, Wajumbe 15 wa Baraza watazingatia idhini ya kile kinachojulikana kama Kifungu cha saba cha mkataba wa Umoja wa Matafa, kinachoruhusu matumizi ya nguvu baada ya hatua zote nyingine za kudumisha amani na usalama kimataifa kutumika vyema”.

Wakati huo huo Umoja wa Mataifa unaendelea kuiunga mkono Haiti katika nyanja mbalimbali, Ujumbe wa kisiasa unaojulikana kama BINUH, unaendelea kuunga mkono juhudi za serikali kuimarisha utulivu wa kisiasa na utawala bora, ikiwa ni pamoja na utawala wa sheria.

Mashirika ya Umoja wa Mataifa pia yanatoa msaada wa haraka wa kibinadamu kwa watu walioathiriwa na ghasia, ukosefu wa usalama na majanga ya asili kama vile tetemeko la ardhi la August 2021.

Mashirika hayo yanaunga mkono mamlaka za kitaifa na taasisi za umma katika kurejesha mafanikio ya muda mrefu ya maendeleo endelevu, ikiwa ni pamoja na kuimarisha uchumi shirikishi na usimamizi wa haki, kuhakikisha utoaji na upatikanaji wa huduma za msingi za kijamii na kuboresha usimamizi wa hatari.