Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Mchezo wa Tenisi

Ulimwengu wa tenesi wajipanga kupambana na mabadiliko ya tabianchi:UN

Special Olympics
Mchezo wa Tenisi

Ulimwengu wa tenesi wajipanga kupambana na mabadiliko ya tabianchi:UN

Tabianchi na mazingira

Mashindano makubwa kabisa manne ya mpita wa tenesi duniani yashikamana kupambana na mabadiliko ya tabianchi kwa kujiunga na mkkati wa kimataifa wa kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi katika michezo.

Ahadi ya ulimwengu wa tenesi ina thamani kubwa katika mkakati huu, tunamuhitaji kika mmoja, tunahitaji kuleta pamoja juhudi za sekta zote katika jamii, juhudi za sekta ya biashara, ulimwengu wa michezo, lakini pia ulimwengu wa tenesi” amesema mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa yenye jukumu la kupambana na mabadiliko ya tabianchi (UNFCCC) Patricial Espinosa.

Katika zama hizi za dharura ya mabadiliko ya hali ya hewa ni lazima tukusanye nguvu zetu pamoja na kuchagiza hatua chanya.”

Kwa mujibu wa UNFCCC Jumanne wiki hii mashindano ya tenesi ya US open ya nchini Marekani na Wibledon ya Uingereza yametangaza kuwa wanajiunga na mkakati wa kudhibito mabadiliko ya tabianchi yakifuatiwa na jana Jumatano mashinadno ya Austalia Open yakathibitisha kufuata nyayo.

Na sasa wakati ambapo mashindano ya French Open ya Ufaransa maarufu kama Roland-Garros yakiendelea , shirikisho la mchezo wa tenesi la Ufaransa linaenzi ushirikiano huo katika tukio maalum mjini Paris

sambamba na Umoja wa Mataifa, mashirikisho mengine ya mchezo wa tenesi, wadau muhimu na wafadhili. Akifafanua kuhusu hatua hiyo rais wa shirikisho la tenesi nchini Ufanransa Bernard Giudicelli amesema “Katika zama hizi za dharura ya mabadiliko ya tabianchi tunahitaji kukusanya nguvu zetu na kuchagiza hatua chanya tukiungana na matukio mengine, nafikiria hususan mashindano makubwa manne ya tenesi pamoja na wachezaji, washirika na wadau wetu wote”

Nyota wa tenisi serena williams akijiunga na kampeni ya kimataifa ya malengo ya maendeleo endelevu ambayo moja wapo ni kupambana na mabadiliko ya tabianchi
@global goals
Nyota wa tenisi serena williams akijiunga na kampeni ya kimataifa ya malengo ya maendeleo endelevu ambayo moja wapo ni kupambana na mabadiliko ya tabianchi

Lengo la mkakati wa mabadiliko ya tabianchi

Mkakati huo wa mabadiliko ya tabinchi na michezo una malengo makuu mawili : mosi ni kuweka bayana njia ambayo ulimwengu wa michezo utaitumia kupambana na mabadiliko ya tabianchi na pili ni kutumia sekta ya michezo kama daraja la kuchagiza na kuelimisha kuhusu mabadiliko ya tabianchi na kuhamasisha kuchukua hatua.

Bi espinosa amesema “Hiki ni kitovu cha jitihada za Umoja wa Mataifa kwa ajili ya michezo kwa kutaka kuchukua hatua dhidi ya janga hilo linaloighubika dunia hivi sasa. Umoja wa Mataifa unatoa wito kwa mashirika yote ya michezo kukumbatia ajenda ya mabadiliko ya tabianchi, bila kujali wapi walipo katika jitihada hizo.”

Mambo 5 ya kuzingatia

Wanaotia saini mkakati huo wa hatua  wakiwemo waandaaji wa mashindano matatu makubwa ta tenesi  wanawajibika katika masuala matano muhimu

. kufanya juhudi maalum za kuchagiza uwajibikaji dhidi ya mazingira

. Kupunguza uchangiaji wa mabadiliko ya tabianchi

. Kuelimisha kuhusu hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi

. Kuchagiza matumizi bora na endelevu

. kupigia chepuo hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi kupitia mawasiliano mbalimbali

Umoja wa Mataifa unasema punde masuala haya yatakapobadilika na kuwa hatua yatasaidia kuunganisha mfumo wa hatua za mbadaliko ya tabianchi katika ulimwengu wa michezo na kuhusisha jamii kubwa ambayo itachangia kwa kiasi kikubwa kampeni za mabadiliko ya tabianchi. Na kwamba jamii ya michezo inaweza kuchangia sehemu yake katika kufikia malengo ya mkataba wa mabadiliko ya tabianchi wa Paris.

Naye James Grabert mkurugenzi wa mkakati wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya maendeleo endelevu na mabadiliko ya tabianchi amesema ni mfano mzuri ulioonyeshwa na Roland Garros, Wimbledon, US Open na Australian Open sio tu kwa sekta ya michezo bali pia kwa kila mtu akisisitiza umuhimu wa michezo kama kiungo au chachu ya watu kuchukua hatua.