Mlinda amani wa Zimbabwe ashinda tuzo ya UN ya mtetezi bora mwanajeshi wa masuala ya jinsia 2021
Mlinda amani raia Zimbabwe ambaye hivi karibuni alimaliza kazi yake katika Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini UNMISS, ameshinda tuzo ya Umoja wa Mataifa ya mwanajeshi mtetezi bora wa masuala ya jinsia kwa mwaka 2021.