Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Heko Marynsia kwa ushindi wa tuzo COP28

Heko Marynsia kwa ushindi wa tuzo COP28

Pakua

Marynsia Mangu, mmoja wa washiriki wa COP28 au mkutano wa 28 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi, UNFCCC uliofanyika huko Dubai, Falme za Kiarabu, ambaye ameondoka akiwa amebeba tuzo. Tuzo inayodhihirisha utendaji wake yeye kama Afisa Mtendaji Mkuu wa shirika lisilo la kiserikali la Success Hands Tanzania.  Shirika hili linahusika na kuwajengea watoto tabia ya kupenda kusoma vitabu, tena tangu wakiwa tumboni mwa mama zao. Idhaa ya Umoja wa Mataifa ilitaka kufahamu mengi kutoka kwake ikiwemo ni tuzo gani ameshinda. Ezzat El Feri wa Idhaa ya Umoja wa Mataifa alizungumza naye huko Dubai na kisha Assumpta Massoi akandaa makala hii. Marynsia anaanza kwa kuelezea tuzo aliyonyakua. 

Audio Credit
Anold Kayanda/Assumpta Massoi
Sauti
3'58"
Photo Credit
Marynsia Mangu