Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mradi wa matumizi bora ya ardhi Tanga na Pwani Tanzania ni wa mfano- Jerome Nchimbi

Mradi wa matumizi bora ya ardhi Tanga na Pwani Tanzania ni wa mfano- Jerome Nchimbi

Pakua

Miongoni mwa hatua zinazochukuliwa hivi sasa na Umoja wa Mataifa ni kushirikiana na nchi wanachama katika kulinda, kutunza na kuendeleza ipasavyo vyanzo vya maji wakati huu ambapo matumizi holela ya vyanzo hivyo ni sababu kuu ya madhara ya mabadiliko ya tabianchi. Mathalani kilimo kisichozingatia mipango katika vyanzo husababisha maji kukauka na wakazi kusalia bila maji. Ni kwa kuzingatia hilio basi Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la mpango wa maendeleo, UNDP nchini Tanzania linashirikana na serikali kutekeleza mradi wa matumizi bora ya ardhi kwa kuwapatia hati miliki za kimila za ardhi kwa wananchi katika mikoa ya Tanga na PWani. Mradi unafadhiliwa na mfuko wa mazingira duniani GEF na serikali yenyewe ya Tanzania. Je hadi sasa nini kinafanyika? Sawiche Wamunza, ambaye ni Mkuu wa Mawasiliano wa UNDP Tanzania amezungumza na mtaalamu anayeanza kwa kujitambulisha.

Audio Credit
Sawiche Wamunza/UNDP Tanzania
Audio Duration
4'15"
Photo Credit
UNDP/Sawiche Wamunza