Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

UN News

Ni sisi wanawake tutakaoubadilisha msemo wa adui wa mwanamke ni mwanamke-Jonitha Nitoya Joram

Mabadiliko chanya katika jamii yanaweza kuanzishwa na mtu mmoja tu, hiyo ndiyo imani ya msichana Jonitha Nitoya Joram muhitimu wa Chuo Kikuu ambaye ameamua kuutumia muda wake wa ziada kuwaelimisha wasichana wenzake na wanawake wafanyabiashara nchini Tanzania ambao hawana elimu ya ujasiriamali. Joanitha anatoa wito kwa kila mtu katika jamii kusambaza kwa upendo maarifa aliyonayo ili kuweza kumkomboa kila mmoja katika jamii hususani wale ambao hawakujaliwa kuipata elimu. Arnold Kayanda wa UN News amefanya mahojiano na msichana huyu anayeanza kwa kueleza namna alivyoanza harakati hizo.

Sauti
3'33"
UN News Kiswahili/ Grece Kaneiya

Wanawake wa Zanzibar sasa wameamka katika ujasiriliamali: Barefoot

Ajenda ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo endelevu SDGs inachagiza hatua zichukululiwe na kila mdau kuanzia serikali, makampuni binafsi asasi za kiraia na hata jamii kuhakikisha hakuna anayesalia nyuma ifikapo 2030. Wito huo unaendelea kuitikiwa na kuleta manufaa katika jamii, mfano kisiwani Zanzibar nchini Tanzania chuo kisicho cha kiserikali cha miguu peku au Bare foot College ni moja ya wadau hao kikitoa mafunzo mbalimbali ya ujasiriamali yanayolenga  kumkomboa mwanamke. Miongoni mwa mafunzo hayo ni ya utengenezaji wa paneli za sola.

Sauti
4'11"
UN-Habitat/Julius Mwelu

Mabadiliko ya mitaa yetu ya Mathare yataletwa na sisi wenyewe-Peter Otieno

Ikiwa imesalia miaka takribani kumi ili kufikia mwaka 2030 ambao ndio mwaka uliowekwa na ulimwengu kuwa malengo 17 ya maendeleo endelevu yawe yametekelezwa kikamilifu, juhudi zinaendelea kila kona kuhakikisha lengo hilo kuu linatimia. Mathalani, Kijana mmoja mzaliwa wa Mtaa wa mabanda wa Mathare mjini Nairobi Kenya, Peter Otieno amefanya uamuzi wa kuwaleta pamoja vijana wenzake ili waanzishishe mradi wa kusafisha mazingira ya mtaa wao kutokana na kero za mirundikano ya taka katika kila kona.

Sauti
4'7"
© UNICEF/UN0346146/Diefaga

Jamii inasemaje kuhusu mkataba wa kimataifa wa haki za mtoto?

Makala ya leo imejikita na mkataba wa haki za mtoto duniani uliopitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa miaka 30 iliyopita ukisimamia nguzo kuu nne ambazo ni haki ya kutobaguliwa, kuhakikisha mahitaji yake yanatimizwa, haki ya kuishi na kuendelezwa na haki ya kusikilizwa. Na je tangu kupitishwa kwa mkataba huo, jamii, wazazi na watoto wenyewe wanauelewaje mkataba huo? Na una maana gani kwao? Ungana na Flora Nducha

 

Sauti
5'53"
UN News/Grece Kaneiya

Dhana niliyokuwa nayo kuhusu China ni tofauti na hali halisi-Mwalimu Gichana

Kwa kawaida taarifa kuhusu eneo au nchi hususan kupitia vyombo vya habari vinatoa taswira moja kuhusu eneo au nchi na wakati mwingine pia kuhusu watu wanoishi sehemu tajwa. Lakini mara nyingi inakuwa hiyo sio hali halisi. Na kwa mgeni wetu kwa makala ya leo, mwalimu Joseph Gichana mzaliwa wa Kenya taswira aliyokuwa nayo kuhusu China ni tofauti na hali aliyoshuhudia nchini humo ambako anafanya kazi na kuishi na familia yake. Kulikoni? Ungana na Flora Nducha na mwalimu Gichana akizungumzia maisha ughaibuni.

Sauti
3'50"
UNICEF

Watoto wanasemaje kuhusu mkataba wa kimataifa wa haki za watoto?

Ikiwa leo ulimwengu unaadhimisha siku ya kimataifa ya mtoto,  makala ya Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa inajikita mkoani Morogoro nchini Tanzania ambako watoto wanatoa maoni yao kuhusu siku yao hii na pia mkataba wa kimataifa wa haki za mtoto, CRC,  ambao umetimiza miaka 30 tangu ulipopitishwa.

Siku ya mtoto duniani ilianzishwa mwaka 1954 na huadhimishwa tarehe 20 mwezi Novemba ya kila mwaka ili kusongesha utangamano na ustawi wa kimataifa miongoni mwa watoto wote duniani.

Sauti
3'13"
MINUSMA/Sylvain Liecht

Hakuna kazi ya mwanaume wala mwanamke ni kujitosa tu:Njeri

Miriam Njeri mshona viatu mashuhuri hivi sasa nchini Kenya, anasema hakutarajia kuwa siku moja angekuja kuwa mshona viatu mkubwa na hata kumiliki kampuni, kazi ambayo kwa kawaida au kwa asililimia kubwa inaminiwa kuwa ya wanaume. Baada ya siku moja kutembelea kazi ya rafiki yake anayemiliki duka la kushona viatu aliamua naye kujitosa katika fani ya ushonaji viatu na kwa sasa amepata mafanio makubwa na kudhihirisha wito wa Umoja wa Mataifa wa kuwachagiza na kuwawezesha wanawake kwa kuwapa fursa .

Sauti
3'31"
USGS/NASA

Asante Benki ya Dunia sasa tunaweza kufungua macho yetu- Wakazi Ningxia, China

Suala la kuenea kwa jangwa ni tatizo ambalo linakumba maeneo mbalimbali duniani kutokana na sababu kadhaa ikiwemo ukataji miti hovyo, ufugaji wa kuhamahama na mabadiliko ya tabianchi. Jamii ndio huathirika zaidi kama ilivyo katika eneo moja huko nchini China ambako jangwa lilienea katika enoe kubwa na hata kusababisha wakazi kupoteza njia za kujipatia kipato, na baya zaidi upepo wa jangwani ukiambatana na vumbi ulikuwa  hatari zaidi kwa macho yao. Hata hivyo Benki ya Dunia ilichukua hatua na kuleta kicheko kwa wakazi wa eneo hilo kama anavyosimulia Grace Kaneiya.

Sauti
3'48"
UN News/Grece Kaneiya

Suala la afya lipo pia mkononi mwako kama mkenya-Waziri Kariuki

Hatua zimepigwa katika kuimarisha afya ya mamilioni ya watu, kuongeza umri wa kuishi, kupunguza vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua na vita dhidi ya magonjwa yanayoambukiza. Hata hivyo kwa mujibu wa ripoti ya utekelezaji wa lengo namba tatu la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs la  kuhakikisha afya kwa wote, hatua haziendi kwa kasi inayohitajika dhidi ya magonjwa makubwa kama vile malaria na kifua kikuu. Aidha karibu nusu ya watu wote duniani hawafikii huduma muhimu za afya huku wengi wakiteseka kutokana na ukosefu wa fedha.

Sauti
4'10"
UNFPA

Vijana tutumie fursa ili kufanikisha azimio la Cairo kuhudu idadi ya watu na maendeleo- Restless Development

Mwaka 1994 huko mjini Cairo Misri kulifanyika mkutano wa kimataifa kuhusu idadi ya watu na maendeleo, ICPD ambao uliibuka na azimio lenye mambo makuu manne, ambayo ni elimu kwa wote ifikapo mwaka 2015, kupunguza vifo vya watoto wachanga na watoto, kupunguza vifo vya wajawazito na kuhakikisha kuwa huduma za afya ya uzazi ikiwemo uzazi wa mpango zinapatikana kwa watu wote ikiwemo vijana wa kike na wa kiume.

Sauti
3'52"