Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

UN Photo/Isaac Billy

Tukishikamana tutaweza kulinda mazingira Uganda:Wanahabari

Changamoto za ulinzi wa mazingira ni mtihani unaozikabili nchi nyingi hasa kutokana na umasikini unaochangia wengi kuingia katika shughuli za uharibifu wa mazingira. Umoja wa Mataifa unaendelea kuzihimiza nchi wanachama kuchukua hatua ili kukabiliana na athari za uharibifu wa mazingira ikiwa ni pamoja na kuacha ukataji miti hovyo kwa ajili ya uchomaji mkaa, kuharibiwa kwa vyanzo vya maji na uharibifu mwingine. Nchini Uganda sasa wanahabari wameamua kulishikia bango suala la kuchagiza jamii kuhifadhi mazingira ikiwemo upanzi wa miti.

Sauti
3'44"
FAO

Wafugaji wa nyuki na mafundi seremala Kigoma wapewa mafunzo ili kuboresha mizinga na uzalishaji bora wa asali.

Tarehe 20 ya mwezi huu wa Mei ilikuwa ni siku ya nyuki duniani msisitizo ukiwa katika kutunza wadudu hao wachavushaji wa maua ambayo ni muhimu kwa uzalishaji wa chakula. Makala yetu kwa kina inaangazia ni kwa vipi wafugaji wa nyuki wanaweza kutunza mazingira na wakati huo huo kujipatia kipato kwa njia fanisi zaidi. Hivyo basi tunamulika mradi wa pamoja wa Kigoma unaoendeshwa na mashirika ya Umoja wa  Mataifa likiwemo lile la chakula na kilimo FAO. Hivi karibuni liliendesha mafunzo kwa wafugaji wa nyuki na mafundi seremala ili kuboresha mizinga na uzalishaji wa asali bora.

Sauti
5'31"
UN /Nektarios Markogiannis

Vijana watakiwa kutumia fursa za teknolojia zilizopo katika kujiajiri

Lengo namba  4 la ajenda ya mwaka 2030 ya malengo ya  maendeleo endelevu au SDGs, linahimiza serikali, asasi mbalimbali za kiraia na mashirika kutoa fursa ya  elimu bora na kukuza nafasi za masomo kwa vijana na jamii zote  ili kuweza kutokomeza umasikini .

Nchini Uganda vijana tayari wako mtari wa mbele  kuhakikisha hawabaki nyuma katika suala la kujiendeleza kwa kutumia fursa za ubunifu na teknolojia zilizopo. 

Audio Duration
3'53"
Photo: Msichana Initiative

Mradi wa msichana mmoja baiskeli moja unafanikiwa, tunakusudia kwenda Tanzania nzima-Sara Bedah

Umbali wa kufika shuleni ni moja ya changamoto zinazochangia kukwamisha malengo ya wasichana wengi ya elimu hususani katika nchi nyingi zinazoendelea. Kwa mujibu wa takiwmu za mashirika mbalimbali likiwemo la Umoha wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF na la elimu, sayansi na utamadubni UNESCO umbali wa kufika shuleni unachangia utoro , mimba za utotoni n ahata mafanikio duni katika masomo na hatimaye maishani kwa wasichana.

Sauti
4'14"
UN News/Patrick Newman

Tanzania yachukua hatua kukabili majanga ya asili

Utabiri sahihi wa hali ya hewa ni mojawapo wa nyenzo  muhimu zinazoweza kuokoa maisha na pia kuepusha madhara makubwa yatokanayo na uharibifu wa miundombinu baada ya vimbuga na mafuriko.

Katika malengo ya maendeleo endelevu ,SDGs au ajenda 2030 ,  lengo namba 13 linahimiza serikali na mashirika mbalimbali kuchukua hatua za haraka ambazo zinaweza kukabiliana na madhara ya  mabadiliko ya tabianchi.

Sauti
2'58"
UN Photo/Manuel Elías

Mipango miji ni hatua ya kwanza katika ujenzi wa miji salama

Lengo namba  9 la malengo ya maendeleo ya endelevu ya Umoja wa Mataifa yanayofikia ukomo 2030, linazungumzia  miundombinu yenye mnepo,  kuwekeza katika  sekta 

ya viwanda endevelu, na kukuza ubunifu. katika sekta hiyo Umoja wa Mataifa unazihimiza serikali na asasi mbalimbali za kiraia kuzingatia ubora wa miundombinu ili  kujenga miji iliyo salama na yenye ustawi bora katika  jamii.

Sauti
4'5"
UN News

Kunashuhudiwa mwamko katika kuendeleza kiswahili duniani-Walibora

Katika awamu hii ya pili ya makala ya mwandishi wa riwaya kutoka Kenya ambaye ameandika vitabu ambavyo vinatumika kama vitabu vya kiada katika shule za sekondari nchini humo.

Licha ya kwamba, kwa maneno yake mwenyewe Walibora anasema hakutarajia hilo lakini vitabu vyake kwa mtazamo wa wengi vinatajwa kuchangia watu wengi ndani na nje ya Kenya kuipenda na kuienzi lugha ya kiswahili. Hapa anaanza kwa kelezea matokeo yaliyotokea baada ya kuchapishwa kitabu chake cha kwanza.

 

Sauti
3'33"