Mbele ya sheria watu wote bila kujali rangi, umri au maumbile ni sawa na wanastahili haki sawa
Takriban miaka 70 imepita tangu tamko la haki za binadamu litolewe. Tamko hilo lina ibara 30 lakini leo tunaangazia ibara ya SABA. Ibara hiyo inasema kuwa “Mbele ya sheria watu wote ni sawa na wanastahili haki sawa za kulindwa. Ili kupata uelewa zaidi wa ibara hiyo Siraj Kalyango wa idhaa hii amezungumza na mwanasheria kutoka Tanzania ambaye anaanza kwa kujitambulisha.