COVAW yabadili maisha ya wasichana wa kaunti ya Kwale
Utalii wasifika sana kwa kuinua kipato cha nchi ya Kenya iliyoko Afrika Mashariki. Hata hivyo baadhi ya watalii wawe wa ndani au wa nje wanatumia fursa hiyo kutekeleza mambo yanayokiuka haki za binadamu hususan kufanya biashara ya ngono. Kutokana na umaskini baadhi ya wasichana kwenye kaunti ya Kwale huko Mombasa, wametumbukia katika mtego wa biashara ya ngono au hata biashara ya binadamu na kujikuta na madhila makubwa zaidi. Shirika moja la kiraia linalopinga ukatili na ghasia dhidi ya wanawake nchini Kenya, COVAW limechukua hatua. Je ni hatua gani?