Biashara ndogo ndogo na mchango wake katika fursa za ajira
Juni 27 ni siku ya kimataifa ya biashara ndogo ndogo na zile za wastani.
Juni 27 ni siku ya kimataifa ya biashara ndogo ndogo na zile za wastani.
Katika neno la wiki hii leo tunaangazia maneno songobingo, sokomoko na segemnege. Mchambuzi wetu ni Nuhu Zuberi Bakari, ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA.
Nchini Kenya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limeibuka na mbinu mpya ya kuwezesha wakimbizi kuondokana na tabia ya baadhi ya watu kuwaona wao si binadamu kwa kuwa ni wakimbizi.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ameshiriki mkutano wa kimataifa kuhusu Cyprus na kuonyesha kuwepo na matumaini kwa nchi hiyo kurejea tena katika taifa moja.
Takribani watu milioni mbili nchini Sudan Kusini wako hatarini kukumbwa na njaa kali licha ya tangazo la hivi karibuni kuwa njaa si tishio tena katika baadhi ya maeneo nchini humo.
Idadi ya raia wa Syria wanaoishi ukimbizini nje ya nchi yao au wale walio wakimbizi wa ndani imeripotiwa kuimarika.
Wakati mzozo wa Sudan Kusini ukizidi kushika kasi, katika mji mdogo uitwao Bunj,uliopo jimboni Uppern Nile, nuru inaangaza kwani msimu wa mvua umeleta ahueni kutokana na maporomoko ya maji yanaleta uzima kwa nyasi na mazao ambazo awali zilikauka.
"Africa Shares" ni jukwaa la kimataifa la kutambua michango ya wakimbizi katika uchumi wa nchi zinazowahifadhi.
Umoja wa Mataifa umesema shambulio la gruneti dhidi ya msafara wa watendaji wake nchini Libya jana Jumatano halitateteresha azma ya kusaidia kusaka suluhu ya amani ya kudumu nchini humo.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limeonya juu ya hatua yoyote ya kuwalazimisha wakimbizi wa Nigeria walioko nchini Cameroon kurejea makwao.