Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Guterres asikitishwa na vifo vilivyotokana na mafuriko Afghanistan

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres
UN Photo/Mark Garten
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres

Guterres asikitishwa na vifo vilivyotokana na mafuriko Afghanistan

Tabianchi na mazingira

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema amesikitishwa na Maisha ya watuyaliyopotea kutokana na mafuriko makubwa watu katika Mkoa wa Baghlan, kaskazini mashariki mwa Afghanistan.

Kupitia taarifa fupi iliyotolewa na msemaji wake mjini New York Marekani hii leo Katibu Mkuu aeleza mshikamano wake na watu wa Afghanistan na pia ametuma salam za rambirambi kwa familia za waathiriwa na amewatakia ahueni ya haraka waliojeruhiwa katika janga hilo. 

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP kupitia chapisho lake Kwenye mtandao wa kijamii wa X limesema mafuriko hayo yamekatili Maisha ya watu zaidi ya 300 na kusambaratisha nyumba zaidi ya 1000.

WFP inasema mafuriko haya ni moja ya matukio mengi ya mafuriko katika wiki za hivi karibuni yanayotokana na mvua kubwa zisizo za kawaida na hivi sasa shirika hilo linagawa biskuti za kuongeza nguvu kwa manusura wa mafuriko hayo.

Katibu Mkuu amesisitiza kuwa Umoja wa Mataifa na washirika wake nchini Afghanistan wanashirikiana na mamlaka husika ili kutathmini kwa haraka mahitaji na kutoa msaada wa dharura unaohitajika .