Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kwa hatua madhubuti twaweza kiutokomeza NTDs: WHO

Wakazi wakisubiri kufanyiwa uchunguzi wa ugonjwa wa Lymphatic Filariasis na Onchocerciasis huko Muheza, Tanzania.
© CDC Global Health
Wakazi wakisubiri kufanyiwa uchunguzi wa ugonjwa wa Lymphatic Filariasis na Onchocerciasis huko Muheza, Tanzania.

Kwa hatua madhubuti twaweza kiutokomeza NTDs: WHO

Afya

Leo ni siku ni siku ya magonjwa ya kitropiki yaliyopuuzwa duniani. Katika ujumbe wake wa siku hii Mkurugenzi mkuu wa shirika la afya duniani WHO Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema, “Magonjwa ya kitropic yaliyopuuzwa au NTDs yanaathiri zaidi ya watu bilioni moja duniani kote hususani katika jamii masikini na zilizotengwa, lakini magonjwa ya NTDs yanazuilika na mara nyingi yanaweza kutokomezwa kabisa katika nchi.”

Dkt. Tedros amesema hadi kufikia sasa takriban nchi 50 zimeweza kutokomeza japo moja ya magonjwa ya NTDs na Dunia iko mbioni kufikia lengo la nchi 100 ifikapo mwaka 20230.

Amesisitiza kuwa “Huduma za afya peke yake hazitoshi kutokomeza magonjwa hayo ni lazima lkushughulikia miziz ambayo ni pengo la usawa linalochochea kuendelea kwa magonjwa hayo ikiwemo unyanyapaa na ubaguzi.”

Maudhui ya mwaka 2024

Kwa mujibu wa WHO maudhui ya siku ya mwaka huu ni “Ungana, kuchua hatua na tokomeza” NTDs, na leo na kila siku WHO inafanyakazi kote duniani ikiungana n anchi na jamii kuchukua hatua na kutokomeza NTDs.

Mkuu wa WHO ametoa wito kwa kila mtu wakiwemo viongozi na jamii kuungana na kuchukua hatua kushughulikia pengo la usawa linalochochea magonjwa hayo. Miongoni mwa magonjwa ya NTDs ni homa ya kidingapopo, Chagas, Matende, Mabusha na vikope.

Dhumuni la siku hii

Madhumuni ya Siku ya Magonjwa ya Kitropiki Yaliyopuuzwa Duniani ni kuchagiza na kuelimisha kuhusu magonjwa ya kitropiki yaliyopuuzwa, mateso yanayosababishwa na magonjwa hayo, kupata msaada wa kuyadhibiti na kuyatokomeza, kulingana na malengo ya programu yaliyowekwa katika ramani ya njia ya kutokomeza  NTDs ya 2021-2030 na ahadi za azimio la Kigali la 2022 kuhusu magonjwa ya tropiki yaliyosahaulika.

Tarehe 31 Mei 2021, Baraza la78 la Afya Ulimwenguni lilitambua tarehe 30 Januari kama Siku ya Magonjwa ya Kitropiki Duniani Yaliyopuuzwa kupitia muafaka wa kauli moja ya uamuzi wa Baraza la Afya Duniani kikao cha 74 WHA74(18) na nchi wanachama wa WHO. 

Siku hii sasa ni mojawapo ya Siku 11 za Afya Duniani na Wiki 2 za Afya Duniani zinazotambuliwa na WHO.